Wahouthi wazishambulia meli za Marekani kwa droni
4 Desemba 2023Matangazo
Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamethibitisha kufanya mashambulizi mawili ya makombora yaliyozilenga meli tatu za kibiashara kwenye Bahari ya Sham.
Tukio hilo linaashiria kuongezeka kwa mfululizo wa mashambulizi ya baharini katika Mashariki ya Kati yanayohusishwa na vita vya Israel na Hamas.
Soma zaidi: Meli ya kivita ya Marekani yazuia mashambulizi ya Wahouthi
Iran, ambayo inatuhumiwa kuliunga mkono kundi la waasi wa KIhouthi nchini Yemen, mpaka sasa haijasema chochote kuhusiana na mashambulizi hayo.
Kwa upande wake, Marekani ilisema ingechukuwa hatua zote zinazohitajika kujibu mashambulizi dhidi yake.