SiasaIran
Wairan kumzika Ayatollah Ali Khamenei nyumbani kwake Masshad
9 Julai 2026
Matangazo
Mazishi ya kiongozi huyo mkuu wa zamani yanafuatia ibada za maombolezo zilizodumu kwa siku kadhaa na kuhudhuriwa na mamilioni ya waombolezaji katika miji mbalimbali nchini Iran na Iraq.
Ali Khamenei aliuawa Februari 28, siku ya kwanza ya mashambulizi ya Marekani na Israel nchini Iran yaliyochochea vita hivyo.
Baada ya maandamano makubwa ya mazishi yaliyopita katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala nchini Iraq siku ya Jumatano, mwili wake ulitarajiwa kufikishwa katika makazi yake ya mwisho katika mji mtakatifu wa Mashhad.
Gavana wa Mashhad, Hassan Hosseini alinukuliwa na televisheni ya serikali akisema kuwa "anatarajia watu milioni 15” kuhudhuria mazishi hayo ya Khamenei.