1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wairani washiriki Ijumaa ya kwanza tangu kuanza kwa vita

6 Machi 2026

Maelfu ya watu walijitokeza kwenye miji kadhaa nchini Iran leo kwa ibada ya kwanza ya Ijumaa tangu kuanza kwa vita baada ya Marekani na Israel kuishambulia kwa pamoja dola hiyo ya uajemi Jumamosi iliyopita.

Iran Tehran 2026 | Raia wa Iran wakiomboleza kifo cha Kiongozi Mkuu Ali Khamenei
Raia wa Iran wakiomboleza kifo cha Kiongozi Mkuu Ali Khamenei.Picha: AFP

Mikanda ya video iliyochapishwa mtandaoni imeonesha makundi makubwa ya wanaume na wanawake waliovaa nguo nyeusi wakiwa wamekusanya kwa sala ya Ijumaa kwenye msikiti mkuu wa Imam Khomeini katikati mwa mji mkuu, Tehran.

Ulinzi ulikuwa umeimarishwa wakati wa ibada hiyo ambayo pia ni ya kwanza tangu Marekani na Israel zilipomuua Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatolah Ali Khamenei.

Kwenye miji mingine ikiwemo Borujerd na Zahedan umati wa watu wenye bendera za nchi hiyo ulisongamana kuelekea misikitini chini ya kiwingu cha mashambulizi ya anga yanayoendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW