1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Wairaqi waandamana baada ya tukio la kuchoma kwa Qur'an

22 Julai 2023

Vikosi vya usalama vya Iraq vimewatawanya takriban wafuasi 1,000 wa kiongozi wa dini ya Kiislamu wa jamii ya Shia, Moqtada Sadr ambao walijaribu kuandamana hadi katika makaazi ya mabalozi wa kigeni mjini Baghdad.

Kontroverse über Koranverbrennungen in Schweden
Picha: Sobhan Farajvan/Pacific Press Agency/IMAGO

 Wafuasi hao wamefanya maandamano hayo wakiamini kuwa Qur'ani ilinajisiwa nchini Denmark.

Baadhi ya waandamanaji walibeba picha za Sadr, ambaye ana ufuasi wa mamilioni ya watu miongoni mwa Washia walio wengi nchini humo na ana ushawishi mkubwa katika siasa za kitaifa.

Soma pia: Iraq yamfukuza balozi wa Sweden

Vikosi vya usalama vilifunga madaraja mawili kuelekea eneo lenye ulinzi mkali la Green Zone ambako kuna taasisi za serikali na balozi za kigeni.

Kulingana na afisa mmoja katika wizara ya mambo ya ndani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina waandamanaji hao walijaribu kupita kwa nguvu kabla ya maafisa kuwazuia na hatimaye waliondoka saa chache baada ya kuibuka malumbano.

Mapema leo wizara ya mambo ya nje ya Iraq ililaani kudhalilishwa kwa Qur'ani takatifu na bendera ya Iraq mbele ya ubalozi wa Iraq nchini Denmark.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW