1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu kote duniani wanaadhimisha Eid al adha

31 Julai 2020

Waislamu kote duniani hii leo wameadhimisha sikuukuu ya Eid al adha, ikiambatana na ibaada ya kuchinja wanyama, katika kuhitimisha ibaada ya Hijja, ambayo ndiyo nguzo ya tano ya Uislamu.

Afghanistan Eid - Adha Opferfest in der Khost Provinz
Picha: DW/F. Zahir

Waislamu kote duniani hii leo wameadhimisha sikuukuu ya Eid al adha, ikiambatana na ibaada ya kuchinja wanyama, katika kuhitimisha ibada ya Hijja, ambayo ndiyo nguzo ya tano ya Uislamu.  Hata hivyo sherehe hizo zimegubikwa na kiwingu cha Corona kinachowalazimu wahusika kuchukua tahadhari zaidi za usafi. Ili kupata picha kamili, 

Soko la Kiamaiko huwa na pilkapilka nyingi katika siku kama ya leo ya Eid al adha ya kuchinja. Sherehe hizo huambatana na mafunzo ya maandiko ya jinsi Mtume Ibrahim aliyekuwa tayari kumtoa mwanawe Ismail kama sadaka kwa kuifuata amri ya Mwenyezi Mungu.Ili kuitimiza ibada hiyo, waislamu kote ulimwenguni huchinja kati ya Ngamia, Ng'ombe, Kondoo au Mbuzi na kugawa sehemu ya nyama hiyo kwa jamaa, marafiki na watu wasiojiweza katika jamii.

Sikukuu hii huangukia siku ya 10 ya mwezi wa kumi na mbili na wa mwisho kwenye kalenda ya kiislamu.Hata hivyo safari hii, kiwingu cha maambukizi ya covid 19 kimeigubika sikukuu ya kuchinja na kuwalazimu waislamu kubaidili mienendo yao.

Barakoa na sherehe za Eid Kenya.

Shughuli ya kuchinja mnyama AfghanistanPicha: DW/F. Zahir

Kwa mujibu wa wizara ya afya nchini Kenya,kila mmoja anatakiwa kuvaa barakoa na kujizuwia kusogeleana kwenye shughuli za kila siku ili kuupunguza uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa wa covid 19. Wiki hii, wizara ya usalama wa taifa iliitenga siku hii rasmi kuwa sikukuu kuwapa wakenya nafasi ya kusherehekea.Wakati huohuo,kwa waislamu wanaojiweza kote ulimwenguni,hiki ndicho kipindi cha ibada ya hajj mjini Mecca nchini Saudi Arabia.

Maandalizi ya Eid Dar es Salaam

01:55

This browser does not support the video element.

Kwa mwaka huu, mambo yamekuwa tofauti kutokana na janga la covid-19, ambapo hakukuwa na mahujaji kutoka nje ya Saudi Arabia, na badala yake, ibaada hiyo imehudhuriwa na raia wa mataifa mbalimbali waliokuwepo tayari nchini humo. Hata miskitini sheria kali zilizotangazwa za kutosegeleana zilitimizwa hapa Nairobi.Hussein Mohamed ni mkaazi wa Kiamaiko na anaelezea jinsi mambo yalivyobadilika miskitini mwaka huu.


Ifahamike kuwa wanyama wanaochinjwa kwa siku ya leo lazima watimize vigezo vya kuwa halal na walio wa kiwango cha juu cha ubora na umri makhsusi.Wasioweza kuchinja kivyao wanaweza kuungana na wenzao na kushiriki katika kumchinja mnyama mmoja mkubwa ambaye ni ama Ngamia au Ng'ombe. Kitamaduni nyama hiyo hugawanywa mara tatu na kutengewa familia,jamaa na marafiki na kwa wasiojiweza kwenye jamii.TM,DW Nairobi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW