Waislamu mjini Paris hufuturu kwa supu ya 'shurba'
14 Septemba 2008Lakini wakati wa mfungo wa Ramadhan harakati zake huongezeka maradu kwa kuwastiri Waislamu wengi wasiokuwa na ajira na wale maskini kwa kuwapatia futari.
Jua linazama katika mji mkuu wa Ufaransa na mamia ya watu waliobanwa na njaa wanajiandaa kufuturu kufuatia adhana ambao ni wito kwa Waislamu kufanya ibada ya sala.
Mahala kwengineko duniani wito huo hutokea moja kwa moja kwenye minara ya misikiti lakini ndani ya hema, moja ya sehemu ngumu ya kaskazini mwa Paris wito huo unatoka kwenye spika ndogo ya radio.
Kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan jiko la supu limefunguliwa nje ya Cite Edmond Michelet ambao ni mradi mgumu wa nyumba katika mamlaka ya wilaya ya 19 ya mitaa yenye sifa mbaya mjini Paris.Katika orodha ya chakula ni chakula cha jadi kinachoanza na mtindi na tende.
Ali Hasni mwenye umri wa miaka 45 ambaye ni mfanyakazi wa kujitolea katika kundi linaloendesha shughuli zake bila ya faida linaloandaa chakula hicho linaloitwa Une Chorba Pour Tous likimaanisha Supu kwa kila mtu anasema siku hizi watu wengi wanashindwa na maisha lakini katu hawatokuambia wewe hayo.
Ufaransa ni maskani ya idadi kubwa ya Waislamu ambao ni wachache barani Ulaya na mjadala juu ya kuwajumuisha Waislamu hao milioni tano katika jamii ya nchi isiojifungamanisha na dini yoyote ile ni mada inayozuka kila mara katika medani ya kisiasa ambapo Waislamu wachache tu hushikilia nyadhifa za kiserikali.
Majengo marefu yanayozunguka hema ni mandhari ya kawaida katika ramani ya miji nchini Ufaransa.
Majengo hayo marefu ambayo mara nyingi hudharauliwa ni maskani ya wahamiaji wengi wa Kiislam ambao walikwenda Ufaransa kufanya kazi wakati wa harakati kubwa za majenzi katika miaka ya 1960 na 1970 kadhalika wahamiaji kutoka dini nyengine.
Mengi ya majengio hayo yalikuwa katika mstari wa mbele katika vurugu za mwaka 2005 wakati vijana wengi wa wahamiaji walipofanya ghasia nchini kote Ufaransa kufuatia kuuwawa kwa kurushwa na umeme kwa kwa bahati mbaya vijana wawili waliokuwa wakikimbizwa na polisi.Tokea wakati huo ghasia zimekuwa zikizuka katika vitongoji vingi vya aina hiyo.
Mamlaka ya wilaya ya 19 inaongoza kwa kiwango cha uhalifu mjini Paris lakini wapika supu wa mitaa hiyo hawakatishwi tamaa na sifa mbaya ya wilaya yao.
Wakati mapigano kati ya makundi ya Kiislamu ya Kiarabu na yale ya Kiyahudi yamekuwa yakihodhi magazeti ya kienyeji katika wilaya ya 19 kila baada ya miezi michache baadhi ya wakaazi wanasema hali ya mvutano imedhibitiwa.
Hema hilo ambalo hujulikana kama eneo kuu limesambaa kwenye viwanja kadhaa vya mpira wa kikapu na wengi wanaoingia kwenye hema hilo ni wanaume na wengi huzungumza Kiarabu.
Chakula kikuu ni mchuzi wa viungo ambao huliwa ukiwa katika aina mbali mbali huko Afrika Kaskazini, Mashariki ya Kati,Ulaya ya Kusini,Uturuki na India. Hapa mchuzi huo huitwa chorba ikiwa tafsiri ya Kifaransa kwa neno la Kiarabu supu.
Kumdi la Une Chorba Pour Tous ambalo kwa kiasi kikubwa huwakusudia Waislamu maskini ilmekuwa likiendesha shughuli zake tokea mwaka 1992. Bajeti yake ya euro 150,000 kwa mwaka kutoka michango ya watu binafsi na ruzuku za wananchi huliwezesha kutowa milo 700 kwa siku kwa kipindi cha mwaka mzima.
Lakini huwa na kazi nyingi sana wakati wa mwezi wa Ramadhan ambapo kwa wastani hutowa milo 2,000 kwa usiku mmoja.
Sadaka ni wajibu wa kidini kwa Uislamu na inakuwa muhimu zaidi wakati wa mwezi huu wa Ramadhan.
Wale wanaojitolea kwenye kundi hilo wanasema watu wengi wanaokwenda kwenye hema sio wale wazururaji lakini ni wahamiaji maskini au wasiokuwa na ajira ya kudumu ambao kuliko chochote kile huwa wanayakosa maisha ya kijamii.