1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Waislamu waadhimisha sikukuu ya Eid al Adha

Sylvia Mwehozi
28 Juni 2023

Waumini wa dini ya Kiislamu leo wanaadhimisha sikukuu ya Eid al Adha, inayofanyika baada ya kumalizika kwa ibada muhimu ya Hajj katika mji mtakatifu wa Makkah, nchini Saudi Arabia.

Afghanistan | Eid Feierlichkeiten
Waumini wa dini ya kiislamu wakiswali swala ya Eid Kandahar, Afghanistan.Picha: Sanaullah Seiam/AFP/Getty Images

Sherehe za Eid al Adha zinaadhimishwa ulimwengu kote, huku waumini waliopata uwezo wa kifedha wakiamrishwa kuchinja mnyama na kutowa sadaka kukumbuka kitendo kilichofanywa na Nabii Ibrahim, cha kuonyesha utayari wa kumchinja mwanawe wa kiume kwa amri ya Mola wake.

Hii leo, mahujaji wanashiriki zoezi la ishara la kumpiga mawe shetani wakati waumini wengine ulimwenguni wakishehereka sikukuu ya Eid inayojumisha uchinjaji wa wanyama.