1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUswisi

Waislamu waghadabishwa na kisa cha kukanyagwa Quran

21 Julai 2023

Mataifa mengi ya Kiislamu yameelezea ghadhabu yao kufuatia kisa cha kukanyagwa hadharani kitabu kitukufu kwa waislamu, Quran nchini Sweden.

Libanon Beirut | Proteste gegen Koran-Schändung in Schweden
Picha: Bilal Hussein/AP/picture alliance

Katika baadhi ya mataifa kulifanyika maandamano baada ya swala ya Ijumaa kuonyesha ghadhabu yao.

Nchini Iran, Iraq na Lebanon, waandamanaji walipanga kuandamana baada ya mhamiaji mmoja kutoka Iraqi anayeishi Sweden kupewa kibali na polisi cha kufanya maandamano na kushuhudiwa akikanyaga nakala ya kitabu cha Quran, nje ya ubalozi wa Iraq.

Soma pia: Iraq yamfukuza Balozi wa Sweden kufuatia kisa cha "kunajisiwa" Quran

Waziri mkuu wa Iraq, Mohammed Shia al-Sudani ameagiza kufukuzwa kwa balozi wa Sweden nchini humo na mwakilishi wao nchini Sweden kurudishwa nyumbani, wakati kundi la wanamgambo wa Shia nchini Lebanon la Hezbollah likiitisha maandamano na kiongozi wake Hassan Nasrallah akiwataka Waislamu kushinikiza serikali zao kuwafukuza mabalozi wa Sweden.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW