1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu wajitayarisha na Eid-ul-Adh'ha

27 Juni 2023

Mamilioni ya Waislamu duniani wanajitayarisha kwa sherehe za sikukuu ya Eid-ul-Adh'ha zitakazofanyika kesho, ikiwa ni ishara ya kukamilika kwa ibada ya Hijja kwenye mji mtakatifu wa Makkah nchini Saudi Arabia.

Saudi Arabien Hadsch Islam Pilgerfahrt
Picha: Amr Nabil/AP/picture alliance

Hii leo mamia kwa maelfu ya mahujaji walikusanyika kwa ibada katika eneo la Mlima Arafa ikiwa ni kilele cha Hija ambayo ni moja ya nguzo kuu tano za dini ya Uislamu.

Licha ya hali ya joto kali, waumini hao walisimama kwenye viwanja vya Arafa kuomba dua, eneo ambalo inaaminika Mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho kwa umma wa Waislamu. 

"Nina furaha sana kufanya ibada ya Hijja. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu. Hatutamani kuondoka eneo hili la (Mlima Arafa). Tizama umma wote huu unashiriki Hijja, tunajihisi tumetakasika." Alisema Samaher al Faisal, hujaji kutoka nchini Syria.

Hapo kesho, mahujaji watashiriki zoezi la ishara la kumpiga mawe shetani wakati waumini wengine ulimwenguni wakishehereka sikukuu ya Eid inayojumisha uchinjaji wa wanyama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW