1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waislamu washerehekea Eid al-Fitr

13 Mei 2021

Waislamu wanashereherekea sikukuu ya Eid al-Fitr katika hali isiyo ya kawaida kwa mwaka wa pili mfululizo, wakati janga la COVID-19 likiendelea kulazimishwa kufungwa kwa misikiti na kutenganishwa kwa familia.

Bildergalerie Fastenbrechen Pakistan Karatschi Eid al-Fitr
Picha: Akhtar Soomro/REUTERS

Kwenye Ukanda wa Gaza  katika mamlaka ya Wapalestina ulioghubikwa na vurugu, wito wa sala Eid unasikika katika majengo yalivunjika na kujaa vifusi wakati ndege za kivita za Israeli zikiendelea kufanya mashambulizi katika vurugu mbaya zaidi tangu vita vya 2014. Soma zaidi Waislamu waadhimisha Eid-ul-Fitr

Kundi la wanamgambo wa Kiislam linalotawala Gaza, Hamas, liliwahimiza waumini

Kuswali sala za pamoja ndani ya nyumba zao au misikiti iliyo karibu na epuka kuwa nje katika maeneo ya wazi. Soma Hamas yakabiliana tena na wanajeshi wa Israel mjini Gaza

Waumini wajumuika kwa sala ya Eid

Picha: Abdullah Rashid/REUTERS

 Waumini waliovalia barakoa walijumuika mitaani katika mji mkuu wa Indonesia, Jakarta.

Mataifa yenye idadi kubwa ya waumini wa kiisalam yameruhusu sala ndani ya misikiti katika maeneo yenye hatari ndogo, lakini misikiti katika maeneo ambayo kulikuwa na hatari zaidi ya kuenea kwa virusi yalifunga hii ikiwa ni pamoja na Msikiti Mkuu wa Istiqlal wa Jakarta, ambao ni mkubwa zaidi Asia ya Kusini-Mashariki.

Huko Bangladesh, makumi ya maelfu ya watu wamekuwa wakiondoka kutoka kwa mji mkuu, Dhaka, kujumuika na familia zao vijiji kwa Sherehe za Eid licha ya vizuizi kwa nchi nzima na vituo vya ukaguzi wa barabara. Wataalam, wanahofia kuongezeka kwa maambukizo nchni humo wakati wakikabiliwa na uhaba wa chanjo. Soma  Miili kadhaa yagunduliwa kwenye mto India

Rais wa Indonesia Joko Widodo kupitia vyombo vya habari amewataka wananchi wa taifa hilo kuzingatia usalma zaidi badala ya kusafiri vijijini.

Vigezo vya kudhibiti maambukizo mapya

Sherehe za Eid AfghanistanPicha: Rahmat Gul/AP Photo/picture alliance

Nchini Malaysia Waziri mkuu Muhyiddin Yassin alitangaza vizuizi vya kutotoka nje kuanzia Jana Jumatano hado Juni 7 ili kukabiliana na ongezeko la maambukizo mapya.

Huku hayo yakijiri makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku tatu kati ya kundi la Taliban na serikali ya Afghanistan yameanza kutekelezwa leo Alhamisi wakati nchi hiyo ikisherehekea siku kuu ya Eid al-Fitr baada ya wiki kadhaa za vurugu.

Makubaliano hayo yaliyopendekezwa na wanamgambo wa Taliban na kuendana na Rais Ashraf Ghani, amani imeleta furaha kwa Waafghanistan wakati wa maadhimisho pamoja na jamaa na rafiki.

 

Vyanzo/AP, AFP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW