1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Waislamu129 wakamatwa mashariki mwa Pakistan

17 Agosti 2023

Polisi wamewakamata Waislamu 129 mashariki mwa Pakistan walioshambulia makanisa na nyumba za Wakristo ambao ni wachache nchini Pakistan.

Pakistan | Angriffe auf Kirchen in Jaranwala
Picha: K.M. Chaudary/AP Photo/picture alliance

Watu hao waliokuwa na hasira walitenda makosa hayo kutokana na kitabu chao cha dini, Quran kukashifiwa. Wakristo wanaoishi katika jiji la Jaranwala kwenye wilaya ya Fais ala bad, walikimbilia kwenye maeneo ya usalamabaada ya Waislamu hao kufanya ghasia.

Hakuna taarifa juu ya majeruhi kutokana na mashambulio hayo ya uharibifu mkubwa kuwahi kufanywa dhidi ya Wakristo. Hata hivyo, kanisa moja lilichomwa moto.

Soma pia:Wairaqi waandamana tena baada ya tukio la kuchoma kwa Qur'an

Mengine manne yaliharibiwa na nyumba kadhaa pia zilichomwa moto na nyingine ziliharibiwa. Wajumbe wa viongozi wa Kiislamu waliwasili kwenye mji wa Jaranwala kusaidia kutuliza hali, huku polisi na wanajeshi wakifanya doria.

Viongozi wa mji wamezifunga shule na ofisi na wamepiga marufuku maandamano kwa muda wa  wiki ili kuzuia ghasia.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW