1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Wajapani wapokea Tuzo ya Amani ya Nobel kwa machozi

12 Oktoba 2024

Shamrashamra zimetanda kote nchini Japan, baada ya Kamati ya Nobel ya Norway kulitangaza kiongozi wa kundi la manusura wa mabomu ya atomiki nchini Japan, Nihon Hidankyo, mshindi wa mwaka huu wa Tuzo ya Amani ya Nobel.

Japan Hiroshima | Toshiyuki Mimaki
Toshiyuki Mimaki, mwanzillishi mwenza wa kundi la wahanga wa mashambulizi ya nyuklia ya Marekani nchini Japan, Toshiyuki Mimaki.Picha: KYODO/REUTERS

Katika tangazo lake la jana, Kamati hiyo ilisema kundi hilo la manusura limechaguliwa kupewa tuzo hiyo kwa juhudi zao za kupigania dunia isiyo na silaha za nyuklia na kwa kuonesha kwa ushuhuda kwamba silaha hizo hazipaswi kutumika tena.

Marekani iliwauwa kiasi cha watu 140,000 baada ya kuwashambulia kwa bomu la nyuklia mnamo tarehe 6 Agosti 1945 mjini Hiroshima, na kuwauwa wengine 74 mjini Nagasaki siku tatu baadaye.

Soma zaidi: Mshindi wa tuzo ya nobel Nihon Hidankyo apongezwa na ulimwengu

Ingawa mashambulizi hayo, ambayo ndiyo pekee duniani kuwahi kutumia nyuklia, yalifanikiwa kukomesha Vita vya Pili vya Dunia na ukatili wa himaya ya Japan barani Asia, lakini pia yalisababisha madhara makubwa na ya muda mrefu, yakiwemo maradhi yatokanayo na mionzi na saratani kwa manusura waliopewa jina la "hibakusha" nchini Japan.