1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajerumani miongoni mwa waliofariki kwa ajali ya ndege Kenya

28 Oktoba 2025

Watu 11 wengi wao wakiwa watalii wamefariki dunia katika pwani ya Kenya mapema leo baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la Kwale.

Kenia Diani 2025 | Flugzeugabsturz - kenianische Beamte inspizieren die Unfallstelle
Picha: AP Photo/picture alliance

Ripoti zinaarifu kuwa ndege hiyo ilikuwa njiani kuelekea katika mbuga ya kitaifa ya wanyama ya Maasai Mara.

Kulingana na taarifa ya shirika la ndege hiyo Mombasa Air Safari, ndege hiyo ilikuwa imewabeba raia wawili wa Ujerumani, wanane kutoka Hungary pamoja na rubani mmoja raia wa Kenya.

Mamlaka zinasema ndege hiyo imeanguka katika eneo lenye milima na misitu lililoko karibu kilomita 40 kutoka uwanja mdogo wa ndege wa Diani.

Mamlaka zinachunguza chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo ingawa inaripotiwa kuwa kulikuwa na mvua kubwa katika eneo la pwani ya Kenya wakati ndege hiyo ilipoanza safari yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW