Wajerumani walio nje wamehimizwa kupiga kura Februari 23
28 Desemba 2024Matangazo
Duru zinaeleza maombi ya usajili tayari yanaweza kuwasilishwa kwa mamlaka za ndani. Wajerumani wanaoishi nje ya nchi wamewekwa katika kundi la raia ambao hawajasajiliwa nchini Ujerumani. Jana Ijumaa, Rais wa UjerumaniFrank-Walter Steinmeier alivunja bunge na kuitisha uchaguzi wa mapema Februari 23, ikiwa ni miezi saba kabla ya tarehe iliyopangwa awali. Uamuzi huo unatokana na kuporomoka kwa muungano wa vyama vitatu uliyokuwa inaongozwa na Kansela Olaf Scholz mwezi Novemba na kufuatiwa na kura ya imani Desemba 16.