1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUjerumani

Wajerumani weusi wahofia ushindi wa chama cha AFD

30 Agosti 2024

Chama cha mrengo mkali wa kulia wa Alternative für Deutschland kimekuwa chama kinachoongoza kueleke uchaguzi wa majimbo ya mashariki mwa Ujerumani ya Saxony na Thuringia, na kuzusha hofu miongoni mwa wahamiaji wengi.

Ujerumani | Haki za Binadamu | Siasa | Bango la AFD
Bango la kuomba kura la AFD likiwa na mjerumani mwenye asili ya AfrikaPicha: Karina Hessland/Imago Images

 Hofu kubwa imetanda zaidi hasa miongoni mwa watu weusi wanaojiuliza iwapo kura zaidi kwa chama hicho zitamaanisha ubaguzi zaidi pia. 

Ulikuwa usiku wa kuliwaza wa majira ya kiangazi mwaka 2020, vizuwizi vya kwanza vya UVIKO-19 nchini Ujerumani vilikuwa ndiyo kwanza vimeondolewa, wakati Omar Diallo na marafiki zake wawili walipotaka kusherehehea sikukuu ya Eid-ul-Adha. 

Diallo, mhamiaji kutoka Guinea mwenye umri wa maia 22, aliliambia shirika la habari la Associated Press wakati wa mahojiano mjini Erfurt, mji mkuu wa jimbo la Ujerumani la Thuringia, kwamba yeye na marafiki zake walikuwa wanafurahia maisha, wakicheza muziki, wakibarizi mjini usiku wakati jioni hiyo ilipogeuka msiba. 

Wakati wakipita katikati ya bustani, pembeni ya jengo kubwa kubwa lililochakaa, ghafla wakakumbana na wanaume watatuwaliovalia nguo nyeusi na weupe.

Ghafla hawakuwa tena watatu, lakini watano, saba, kote katika eneo hilo. Hivyo hakukuwa na njia ya kutoroka. Hivyo moja wetu alikamatwa na kupigwa vibaya kiasi kwamba alilazwa kwa siku tatu na hakuweza kufanya chochote.

Soma pia:Utafiti: Ubaguzi wa rangi unachangia umaskini Ujerumani

Diallo hakumbuki kwa muda gani waliwindwa, lakini wakati fulani aliweza kuita polisi, na wakati maafisa waliowasili, washambuliaji walikimbia.

Kuwa mweusi nchini Ujerumani kumemaanisha wakati wote kukabiliwa na hatari ya ubaguzi katika miundo yake yote, kuanzia udhalilishaji wa kila siku hadi mashambulizi ya kudhuru.

Hata hivyo wataalamu wanasema kuwa mweusi Mashariki mwa Ujerumani inamaanisha uwezekano wa kuwa muathirika wa ubaguzi wa rangi unaoweza kuwa hata mbaya zaidi.

Hofu ya watu weusi inahusishwa na historia

Wakati Ujerumani Mashariki ilikumbatia demokrasia, na jamii anuai katika miongo ya baada ya Vita vikuu vya Pili vya Dunia, katika Ujerumani Mashariki iliyokuwa inatawaliwa kidikiteta hadi mwishoni mwa mwaka 1989, wakaazi hawakuwa na fursa chache mno za kutangamana na watu wa makabila mengine, na walikuwa hawaruhusiwi kutembea kwa uhuru nje ya nchi.

Wataalamu wanasema hasa katika jimbo la Thuringia, makundi ya mrengo mkali wa kulia yameunda mazingira ya uhasama kwa wachache, wakiwemo weusi.

Mwaka 2023, shirika lisilo la kiserikali la Ezra, linalowasaidia waathirika wa vurugu za wafuasi wa mrengo wa kulia, ubaguzi na chuki dhidi ya wayahudi, lilirekodi mashambulizi 85 jimboni Thurungia.

Mashambulizi hayo ni chini kidogo tu ya 88 yaliorekodiwa mwaka uliotangulia wa 2022.  Ezra inasema katika miaka ya karibuni, vuguvugu la itikadi kali za mrengo wa kulia limeibuka jimboni Thuringia, na kuchangia mabadiliko makubwa ya kiitikadi kwa wafuasi wake.

Soma pia: Ujerumani yakumbwa na maandamano ya kupinga itikadi kali za mrengo wa kulia

Kisiasa, chama cha Alternative for Germany ndiyo mnufaika mkuu wa hali hii. Ezra na mashirika mengine kadhaa yanayofuatilia ubaguzi wa rangi katika jimbo hilo waliandika katika ripoti ya kila mwaka kuhusu hali katika jimbo hilo lenye wakazi wengi wa mashambani lenye jumla ya watu karibu milioni 2.1.

Uungwaji mkono wa AfD mashariki mwa Ujerumani

03:05

This browser does not support the video element.

Hatua hiyo pia inaonekana katika kura za maoni kuhusu uchaguzi ujao jimboni humo mnamo Septemba 1, ambapo hadi asilimia 30 ya wapiga kura Thuringia walisema wanataka kukipigia kura chama hicho cha AfD, na kukiweka mbele ya vyama vingine vikuu.

Uchaguzi pia unakuja katika majimbo ya mashariki ya Saxony na Brandenburg ambako AfD pia inaongoza katika uchunguzi wa maoni.

Itikadi kali za AFD eneo la mashariki

Tawi la AfD la Thuringia ni la msimamo mkali hasa na liliwekwa chini ya uchuguzi wa idara ya upelelezi wa ndani miaka minne iliyopita, kama kundi lililotibitishwa la itikadi kali za mrengo wa kulia.

Matamshi makali ya chama hicho yameibua siyo tu wasiwasi wanaopambana dhidi ya ubaguzi, lakini pia jamii za wachache kama vile Wajerumani weusi na wahamiaji wa Kiafrika, ambao ni miongoni mwa jamii za wachache zilizo hatarini zaidi, na ambao ndiyo kwanza kubaguliwa. 

Doreen Denstaedt, binti wa Baba wa Kitanzania na Mama Mjerumani mweupe, alizaliwa na kukulia Thuringia. Denstadt mwenye umri wa miaka 46, ni mwanachama wa chama cha Watetezi wa Mazingira cha die Grüne, na waziri wa uhamiaji, sheria na ulinzi wa walaji wa jimbo hilo.

Kama barobaro, hakuruhusiwa kwenda nyumbani kivyake kwa sababu ya uwezekano wa mashambulizi ya kibaguzi dhidi yake, na baadhi ya wakati aliitwa kwa majina ya kibaguzi shuleni kwake.

Anahofia kwamba katika mazingira ya sasa ya kisiasa, simulizi ya kibaguzi zinazozidi kuenezwa zitakubalika katikati mwa jamii na kuchukuliwa kwa wepesi.

"Kwa maneno mengine, kuna hatari kubwa kwamba hii itasababisha hali hii ionekane ya kawaida, kwamba baadhi ya simulizi zitaenea na kuwa za kawaida. Huo ndiyo wasiwasi wangu mkubwa." Alisema.

Watu weusi ni wachache nchini Ujerumani, wameishi nchini humo kwa mamia ya miaka. Haijulikani wazi ni watu wangapi weusi wanaoishi nchini humo kutokana na ukweli kwamba makabila hayaorodheshwi rasmi, lakini kwa mujibu wa makadirio, karibu watu milioni 1.27 wenye asili ya Afrika wanaishi katika taifa hilo la wakaazi milioni 83.

Zaidi ya asilimia 70 kati yao walizaliwa nchini Ujerumani, kwa mujibu wa Mediendienst Integration, ambalo ni shirika linalofuatilia masuala ya uhamiaji nchini Ujerumani.

Ukoloni wa ujerumani Afrika watajwa

Himaya ya Ujerumani ilikuwa na makoloni kadhaa barani Afrika kuanzia mwaka 1884 hadi mwishoni mwa Vita vikuu vya Kwanza vya Dunia.

Makoloni haya yanajumlisha mataifa ya sasa ya Tanzania, Burundi, Rwanda, Namibia, Cameroon, Togo na Ghana. Serikali ya Ujerumani imeanza hivi karibuni tu kushughulikia dhulma zilizofanyika wakati wa kipindi hicho.

Ilikuwa mwaka 2023 ambapo Rais wa Ujerumani aliomba msamaha kwa mauaji ya wakati wa ukoloni nchini Tanzania, zaidi ya muongo mmoja uliyopita.

Mbunge wa Ujerumani mwafrika aliyejizulu sababu ya vitisho

01:52

This browser does not support the video element.

Daniel Egbe, mkemia kutoka Cameoon, aliehamia Thuringia mwaka 1994 kwa ajili ya masomo, alisema alishtushwa na namna Wajerumani wanavyojua kidogo sana kuhusu historia ya ukoloni ya taifa hilo inapokuja kwa watu weusi.

Soma pia:Ubaguzi wa rangi Ujerumani wafichuliwa katika ripoti mpya

Egbe, aliechukuwa uraia wa Ujerumani mwaka 2003, alianzisha shirika la AMAH lenye makao yake mjini Jena katika jimbo hilo la mashariki, na linawasadia wanafunzi wa vyuo vikuu na wahamiaji kutoka Afrika wanapopitia ubaguzi.

Kwa Diallo, mhamiaji kutoka Guinea alieshambuliwa mjini Erfurt miaka minne iliyopita, pia ameahidi kusaidia kuboresha hali ya watu weusi nchini Ujerumani. Ingawa Diallo alisema shambulio hilo lilimtia kiwewe, lakini pia lilimuwezesha kupambania haki zaidi kwa watu weusi nchini Ujerumani.

Mwaka mmoja uliyopita, alijiunga na chuo kikuu mjini Munich kusoma sheria, lakini bado anitembelea Erfurt mara nyingi kuandamana kudaii haki za wahamiaji na kupinga ubaguzi wa rangi.

Wakati Egbe pia ana wasiwasi kwamba chama cha AfD kinaweza kupata nguvu zaidi katika uchaguzi ujao, alisema hataondoka Thuringia licha ya ubaguzi unaozidi.

"Hata kama hali mbaya zaidi itajitokeza, tutabakia hapa. Hatutaondoka na tunapaswa kufanya kila linalowezekana kuibadili jamii hii," alisema Egbe.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW