1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe kushiriki kongamano la mazingira la Colombia

18 Oktoba 2024

Maelfu ya wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili nchini Colombia kwa ajili ya mkutano wa kilele wa mazingira unaojaribu kukomesha uharibifu wa mazingira asilia unaofanywa na binadamu.

Wajumbe karibu12,000 kushiriki kongamano la mazingira la Colombia
Wajumbe karibu12,000 kushiriki kongamano la mazingira la ColombiaPicha: Fernando Vergara/AP Photo/picture alliance

Mkutano huo unafanyika katika mji wa Cali ulio katika hali ya tahadhari kutokana na vitisho vya makundi ya waasi.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya viumbe hai unatarajiwa kuanza Jumatatu chini ya ulinzi mkali wa polisi na wanajeshi wa Colombia wapatao elfu 11 wakisaidiwa na maafisa wa usalama wa Umoja wa Mataifa na Marekani.

Takriban wajumbe elfu 12,000 wakiwemo mawaziri 140 wa serikali na wakuu saba wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria kongamano kubwa zaidi la ulinzi wa mazingira duniani, linalofanyika kila baada ya miaka miwili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW