1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTogo

Wajumbe wa ECOWAS waelekea Togo wakati mivutano ikiongezeka

16 Aprili 2024

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi - ECOWAS imesema ujumbe wake ulitarajiwa nchini Togo wakati mivutano ikiongezeka kuhusu mageuzi ya kikatiba.

Rais wa Togo Faure Gnassingbe
Wapinzani nchini Togo wanasema Rais Faure Gnassingbe anataka kurefusha utawala wake kupitia mageuzi ya katibaPicha: Ute Grabowsky/photothek/IMAGO

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi - ECOWAS imesema ujumbe wake ulitarajiwa nchini Togo wakati mivutano ikiongezeka kuhusu mageuzi ya kikatiba ambayo upinzani unasema yataurefusha utawala wa Rais Faure Gnassingbe.

ECOWAS imesema ujumbe huo utashauriana na wadau wakuu kuhusu matukio ya karibuni zaidi nchini Togo kabla ya uchaguzi wa bunge na majimbo Aprili 29.

Ujumbe huo unaongozwa na Maman Sambo Sidikou, mkuu wa zamani wa ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Mali na Sahel, na utabaki nchini humo kuanzia Jumatatu hadi Aprili 20 kufuatia mwaliko wa serikali.

Mivutano imeongezeka Togo tangu mwezi uliopita, wakati wabunge waliunga mkono mageuzi ya kikatiba yatakayoisogeza nchi hiyo kwa mfumo wa bunge ambapo wabunge ndio watamchamgua rais atakayehudumu kwa muhula wa miaka sita. Upinzani unahofia kuwa ni njama ya kurefusha utawala wa Gnassingbe, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka wa 2005 na kushinda tena katika uchaguzi uliolaaniwa na wapinzani waliosema ulijaa matukio ya udanganyifu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW