Wajumbe wa Isreal na Palestina waanza majadiliano
15 Januari 2008Matangazo
MASHARIKI YA KATI:
Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba,wajumbe wa Israel na Palestina wanaojadiliana wamefanya mazungumzo kuhusu baadhi ya masuala nyeti katika mchakato mzima wa mazungumzo.Masuala nyeti ni kama vile mustakabla wa mji wa Jerusalem,mipika halisi,kujitawala pamoja na hatima ya wakimbizi wa Kipalestina.Majadiliano yamekuja siku chache baada ziara rasmi ya rais George W. Bush nchini Israel na katika maeneo yanayokaliwa ya West Bank.