Wajumbe wa Marekani na Iran waanza mazungumzo Islamabad
11 Aprili 2026
Matangazo
Wajumbe hao wawili walianza mazungumzo ya ana kwa ana leo alasiri chini ya usimamizi wa Pakistan baada ya siku ya mashaka na usiri ambao ulizua uvumi iwapo wajumbe hao watakutana au la.
Kumekuwa na uvumi wa siku nzima ulioashiria kuwa ujumbe wa Iran huenda usikae na ule wa Marekani na kwamba ni ujumbe tu ungetumwa kupitia wapatanishi, Pakistan.
Chanzo kimoja cha ulinzi cha Pakistan kilichozungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, kimeliambia shirika la habari la dpa kwamba mazungumzo hayo yameanza vizuri.
Haya yanajiri huku jeshi la Israel likisema leo kuwa limeshambulia zaidi ya shabaha 200 za Hezbollah nchini Lebanon ndani ya saa 24 zilizopita.