1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa Marekani na Iran wakutana Geneva

17 Februari 2026

Marekani na Iran zafanya mazungumzo chini ya kiwingu cha mivutano mikali kuhusu mpango wa Nyuklia wa Tehran

Jengo la ubalozi wa Oman nchini Usiwi ambako yanafanyika mazungumzo  kati ya Iran na Marekani
Jengo la ubalozi wa Oman nchini Usiwi ambako yanafanyika mazungumzo kati ya Iran na MarekaniPicha: Pierre Albouy/REUTERS

Wajumbe wa ngazi za Juu wa Iran na Marekani wanakutana kwa mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, yanayosimamiwa na Oman mjini Geneva.

Mazungumzo hayo yatakayoendeshwa bila ya kuwakutanisha moja kwa moja wajumbe hao yanafanyika katika ubalozi wa Oman mjini Geneva. 

Tehran imeonesha kuwa tayari kupunguza shughuli za mradi wake wa nyuklia, ikitaka badala yake kuondolewa vikwazo vikali vya kiuchumi.Iran na Marekani kuendeleza mazungumzo Uswisi

Hata hivyo Jamhuri hiyo ya kiislamu pia imeshasema haitokuwa tayari kujadili kuhusu suala la kupunguza idadi ya makombora yake au kuacha kuyaunga mkono makundi ya wanamgambo.

Mazungumzo ya Geneva yanakuja katikati ya mivutano ya wiki kadhaa kati ya mataifa hayo mawili baada ya rais Donald Trump kutishia kuishambulia Tehran  kufuatia hatua ya kuuwawa kwa waandamanaji wanaoipinga serikali ya Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW