1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa Marekani na Ulaya waujadili mzozo wa Ukraine

15 Desemba 2025

Wajumbe wa Marekani wamekutana na wenzao wa Ulaya katika mji mkuu wa Ujerumani - Berlin siku ya Jumatatu kuujadili mpango wa amani unaolenga kuvimaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.

Berlin | Mkutano wa Wajumbe wa Marekani na Ulaya wakiujadili mzozo wa Ukraine
Mkutano wa Wajumbe wa Marekani na Ulaya wakiujadili mzozo wa Ukraine huko BerlinPicha: Christoph Soeder/dpa/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anayehudhuria mkutano huo amesema nchi yake iko tayari kuachana na azma ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO ikiwa itahakikishiwa usalama wake, lakini Kiev imeshikilia msimamo wake wa kutoyaachia maeneo yake kwa Urusi.

Msemaji wa serikali ya Ujerumani Stefan Kornelius amesema uthabiti wa makubaliano yoyote ya amani utategemea hakikisho la usalama litakalotolewa kwa Ukraine na kusisitiza kuwa maslahi ya bara zima la Ulaya yako hatarini na yanahitaji kulindwa. Kwa upande wake,  ujumbe wa Marekani umeelezea kuridhishwa kwake na hatua zilizopigwa hadi sasa katika mazungumzo hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW