1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe wa Marekani wako Israel kwa mazungumzo na Netanyahu

24 Januari 2026

Wajumbe wa Marekani Steve Witkoff na Jared Kushner wamefanya ziara nchini Israel leo kukutana na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Benjamin Netanyahu, kujadili zaidi kuhusu suala la Gaza.

Saudi-Arabia , Riyadh 2025 | Steve Witkoff
Mjumbe Maalum wa Marekani, Steve Witkoff Picha: Evelyn Hockstein/AFP

Msemaji wa ofisi ya waziri mkuu wa Israel amethibitisha kuwa mkutano huo ulipangwa lakini hakutoa maelezo zaidi.

Wakati huo huo, Wizara ya Afya ya Palestina huko Gaza imesema kuwa shambulizi la Israel limewaua watu watatu, wakiwemo watoto wawili katika matukio mawili tofauti kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Taarifa kutoka kwa jeshi la Israel imesema wanajeshi wake wanaofanya operesheni katika eneo la kaskazini mwa ukanda huo waligundua kwamba wanamgambo kadhaa walivuka na kuingia eneo lisiloruhusiwa wakatega kifaa cha kilipuzi katika eneo hilo, na kuwasogelea maafisa hao hali iliyowasababishia hatari.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW