Wajumbe wa UN watembelea Beni, DRC
14 Novemba 2016Matangazo
Ujumbe huo ulikutana kwa mazungumzo na gavana wa mkoa wa Kivu ya Kaskazini pamoja na Meya wa Beni, mkuu wa wilaya ya Beni, kamanda wa jeshi la Serikali katika eneo la mashariki mwa DRC, pamoja na makamanda wa polisi katika mji na wilaya ya Beni. Ujumbe huo ulikutana pia kwa mazungumzo na wajumbe wa mashirika ya kiraia waBeni.