1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wajumbe kushiriki kongamano la mazingira la Colombia

Sylvia Mwehozi
18 Oktoba 2024

Maelfu ya wajumbe kutoka nchi tofauti duniani wameanza kuwasili nchini Colombia kwa ajili ya mkutano wa kilele wa mazingira unaojaribu kukomesha uharibifu wa asili unaofanywa na binadamu.

Mji wa Cali ulioko Colombia
Mji wa Cali ulioko ColombiaPicha: El Tiempo/GDA via ZUMA Press Wire/picture alliance

Maelfu ya wajumbe kutoka nchi tofauti duniani wameanza kuwasili nchini Colombia kwa ajili ya mkutano wa kilele wa mazingira unaojaribu kukomesha uharibifu wa asili unaofanywa na binadamu. Mkutano huo unafanyika katika mji wa Cali ambao upo katika hali ya tahadhari kufuatia vitisho kutoka kwa vikundi vya waasi. Soma: COP15: Bioanuwai ni nini na kwa nini ni muhimu sana?

Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya viumbe hai unatarajiwa kuanza siku ya Jumatatu chini ya ulinzi mkali wa polisi na wanajeshi 11,000 wa Colombia, wakisaidiwa na maafisa wa usalama wa Umoja wa Mataifa na Marekani. Takribani wajumbe elfu 12,000 wakiwemo mawaziri 140 wa serikali na wakuu saba wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria kongamano kubwa zaidi la ulinzi wa mazingira duniani, linalofanyika kila baada ya miaka miwili.