1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makubaliano ya kusitisha uchafuzi wa taka za Plastiki bado

1 Desemba 2024

Mazungumzo kuhusu rasimu ya makubaliano ya kupunguza uchafuzi unaosababishwa na taka za plastiki,yanakaribia kufikia mwisho.

Südkorea Busan | Klimaaktivisten demonstrieren für Plastikmüll-Bekämpfung
Wanaharakati wa mazingira wanaonyesha juhudi za kupambana na taka za plastikiPicha: Minwoo Park/REUTERS

Mataifa ya dunia, yanayoshiriki mazungumzo yamekuwa yakijaribu tangu jana kufikia makubaliano katika vikao vya faragha lakini rasimu ya mkataba iliyotolewa  imeamuwa suala hilo lijadiliwe katika kikao cha wazi baadae leo.Rasimu hiyo inapendekeza uwezekano wa kupigwa marufuku baadhi ya bidhaa za plastiki za kutumika mara moja au zinazotowa kemikali za sumu. Panama na Fiji zimetaka mataifa ambayo hayaungi mkono malengo ya rasimu hiyo yajiweke pembeni,msimamo ambao umeungwa mkono na Mexico,Ufaransa,Rwanda na Umoja wa Ulaya ambazo zimesema kwa pamoja zitafanya kila ziwezalo kushinikiza rasimu hiyo ipitishwe kutatua mgogoro wa uchafuzi unaosababishwa na taka za plastiki.Ghana imeiita rasimu hiyo ya sasa kuwa dhaifu Kumi,ambayo haizilazimishi nchi kusitisha kabisa matumizi ya bidhaa za plastiki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW