1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Wakaguzi wa IAEA wamewasili Iran

22 Februari 2023

Mkuu wa mpango wa nyuklia nchini Iran, Mohammad Eslami, amesema wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Nyuklia, IAEA, wamewasili nchini Iran kwa ajili ya majadiliano na uhakiki.

Iran Atomkraftwerk Buschehr
Picha: ABEDIN TAHERKENAREH/epa/dap/picture alliance

Afisa huyo mwandamizi amesema wakaguzi hao tangu Jumanne wamekwishaanza kazi ya majadiliano na ukaguzina kwamba utata uliosababishwa na wakaguzi umetatuliwa.

Juma lililopita shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye kuratibu shughuli za nyuklia lilisema lipo katika majadiliano na Iran.

Mazungumzo hayo yalikuwa yanafanyika kutokana na matokeo ya hivi karibuni baada ya shirika la habari la Bloomberg kuripoti madini ya urani yamerutubishwa kwa kiwango cha asilimia 84, kikiwa karibu na uundwaji wa silaha za nyuklia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW