1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je pana hatari ya janga la corona kurudi tena Ujerumani?

13 Septemba 2023

Wakati msimu wa kiangazi unamalizika hapa nchini, maambukizi ya virusi vya corona yanaongozeka. Jee pana hatari ya janga la corona kurudi tena nchini Ujerumani?

Symbolbild Coronavirus Selbsttest
Muuguzi akionyesha kifaa cha kujifanyia vipimo vya corona Picha: pressefoto_korb/picture alliance

Janga la corona limemalizika rasmi kwa mujibu wa tangazo la shirika la afya duniani WHO. Vita vya uvamizi vya Urusi nchini Ukraine, hali mbaya ya hewa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na mizozo ndani ya serikali ya mseto ya Ujerumani vimegubika nafasi ya Corona katika vichwa vya habari.

Lakini baadhi ya watu nchini Ujerumani wana wasiwasi kutokana na kuongezeka, idadi ya maambukizi ya virusi vya corona mnamo wiki za hivi karibuni.

Hata hivyo profesa Stefan Kluge mkurugenzi wa hospitali ya wagonjwa mahututi ya mjini Hamburg amesema hakuna haja ya kuwepo wasiwasi. Amesema kwa sasa wapo wagonjwa 182 na nusu ya hao ni wale wenye uvimbe kwenye mapafu kutokana na maambukizi ya corona. 

Ujerumani yakaza sheria za COVID-19 kwenye mabaa na migahawa

Profesa Stefan Kluge ameeleza kuwa hiyo ni asilimia moja tu ya wagonjwa wote waliolazwa kwenye kitengo cha mahututi. Amesema hali ni imara licha ya kuongezeka kwa wagonjwa wenye maambukizi  mnamo wiki za hivi karibuni. Hata hivyo uhaba wa wahudumu kwenye hospitali unaweza kuwa tatizo na hasa katika msimu wa baridi.

Aina mpya ya virusi vya corona zazua wasiwasi wa kuenea kwa ugonjwa wa Uviko 19

Picha inayoonyesha kirusi cha corona Picha: Zoia Fedorova/Zoonar/picture alliance


Kwa mujibu wa taarifa kwa sasa pana aina mbili za virusi vinavyoenea duniani. Kimojawapo kinaitwa Pirola  kilichogunduliwa nchini Denmark,Marekani, Uingereza,Uswisi na Israel. Kwa mujibu wa taaarifa ya chuo cha tiba cha  Robert Koch, aina ya virusi vinavyoitwa Eris vimegundulika nchini Ujerumani.Virusi hivyo tayari vimesababisha kizaizai nchini Marekani. Watu wengi wanaendelea kulazwa hospitali.

Ujerumani kulegeza vikwazo vya kuzuia maambukizi ya corona


Shirika la afya duniani WHO linawasi wasi huenda virusi hivyo vikaenea duniani kote. Hali inaweza kuwa ngumu katika kipindi cha baridi kali nchini katika sehemu kadhaa za Ujerumani kutokana na uhaba wa vitendea kazi. Mbali na maabukizi ya corona yapo magonjwa mengine katika msimu wa baridi.


Wataalamu wa tiba wanahofia watu wengi watakumbwa na maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani katika msimu huo, na hasa wazee na watu wenye magonjwa ya muda mrefu. Mwenyekiti wa shirikisho la madaktari nchini Ujerumani amesema madaktari wengi sasa wanashughulika na watu wenye virusi vya corona.

Kimsingi hilo halipaswi kuwa tatizo lakini madaktari wanasema wanafanya kazi kwa nguvu zao zote. Wizara ya afya hapa nchini, inapaswa kujiweka vizuri kupambana na hatari ya janga jipya la maambukizi ya Corona.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW