1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakatoliki wasubiri kuchaguliwa kwa Papa mpya

7 Mei 2025

Makadinali kutoka sehemu mbalimbali duniani wamejumuika katika misa maalum leo Jumatano katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter mjini Vatican kabla ya kongamano la kumchagua papa mpya.

Vatikani 2025 | Makadinali wakiwa kwenye misa kwa ajili ya kumchagua Papa
Makadinali watajifungia kwa muda hadi pale mmoja miongoni mwao atakapofanikiwa kumpata kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki.Picha: Dimitar Dilkoff/AFP/Getty Images

Misa hiyo inaongozwa na mkuu wa Chuo cha Makadinali, Giovanno Battista Re, kama ibada ya mwisho hadharani kabla ya makadinali hao kushiriki mkutano wa faragha wa kumchagua mrithi wa Papa Francis.

Soma pia: Baraza Maalumu la kumchagua Papa kuanza leo Vatican

Watajifungia kwenye kanisa hilo kwa muda usiojulikana hadi pale mmoja miongoni mwao atakapofanikiwa kupata theluthi mbili ya kura na kutawazwa rasmi kuwa kiongozi mkuu wa kanisa hilo lenye waumini wapatao bilioni 1.4 ulimwenguni kote.

Waumini na wafuatiliaji wengine kote duniani watasubiri ishara ya kuchaguliwa kwa papa mpya kupitia moshi utakaotoka kwenye chimni iliyofungwa juu ya Kanisa la Sistine.

Soma pia: Makadinali wawili kukosa kongamano la kumchagua papa mpya

Moshi mweupe utakapofuka itakuwa ni ishara kuwa baraza hilo la makadinali limefanikiwa kumchagua kiongozi mpya wa kanisa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW