010710 First Ladies Deutschland
2 Julai 2010Kuwa mke wa rais wa Ujerumani , sio kazi na kwa hiyo suala hilo halitajwi katika katiba ya Ujerumani. Lakini ni jukumu, ambalo linapaswa kuangaliwa kwa undani. Bettina Wulff ni, "mama wa kwanza wa taifa" wa kumi, katika historia ya jamhuri ya Ujerumani. Akiwa na Christian Wulff, pamoja na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa miaka miwili pamoja na mtoto kutoka katika ndoa yake ya zamani watahamia katika makaazi ya kasri la Bellevue, mahali wanapoishi marais.
Anataka kuwa kama afisa habari, ikiwa ndio wajibu wake katika wakati rais mume wake atakapotumikia wadhifa wake. Mshukuru mkeo kwa kuwa amekufanyia mengi.
Rais wa zamani wa Ujerumani Horst Köhler amekwishafanya hivyo. Baada ya kuchaguliwa kwake mwaka jana alimshukuru hadharani mkewe Eva Luise Köhler. Familia ya Köhler ilikuwa ni familia iliyokuwa na uhusiano wa karibu sana, ikiwa mkewe ni mtu wa karibu sana anayempa ushauri.
Mwamamume huwa imara pale anapokuwa na mke imara.
Mama wa kwanza wa taifa Bettina Wulff anataka kuchukua mfano wa aina ya Eva Köhlers, wa kuwakaribia watu, na kujishughulisha katika masuala ya kijamii. Amesomea masomo ya uhusiano na umma na akiwa na umri wa miaka 36, Bibi Bettina Wulff anakuwa mke wa kwanza wa rais ambaye ni kijana zaidi na analeta haiba katika kasri la Bellevue. Aina ya maisha yake ya mcheza sinema pamoja na michoro ya tatoo katika sehemu ya juu ya mkono wake imemfanya aandikwe katika magazeti kadha.
Bettina Wulff pia hujishughulisha na masuala ya kijamii. Hali hii inamuweka karibu na wake wa marais waliopita. Wote walijihusisha na huduma za kijamii kwa ajili ya afya ya kina mama na mtoto. Muasisi alikuwa mke wa rais wa kwanza wa Ujerumani Theodor Heuss, ambaye alikuwa akijihusisha pia na masuala ya kisiasa na mageuzi ya kijamii Elly Heuss-Knapp katika mwaka 1950.
Christina Rau, mke wa rais wa zamani Johannes Rau , alikuwa pia akishughulika kama alivyokuwa akifanya bibi yake, ambaye alikuwa ameolewa na rais wa zamani Gustav Heinemann.
Nimeijua jumuiya hii kupitia bibi yangu Hilda Heinemann, ambaye alikuwa pia kiongozi , kwakuwa kulikuwa na aina ya utamaduni, kwamba mke wa rais ni lazima awe kiongozi wa jumuiya hiyo.
Katika mwaka 2000, katika maadhimisho ya miaka 50 ya jumuiya hiyo inayojishughulisha na kuwapa mapumziko wanawake, anasema Christina Rau kumekuwa na ugawanaji majukumu baina ya wanaume na wanawake.
Mzigo mkubwa uliendelea kubakia kwa akina mama. Hali hiyo imebadilika kidogo hata hivyo, lakini takwimu zinaonyesha , kwamba wakati mtoto wa kwanza anapopatikana, kazi alizokuwa akifanya baba nyumbani zinaanza kupungua. Ile ndoto , kwamba hakutakuwa na sababu ya kuwapatia mama na mtoto uangalizi, kwa kuwa mwenza wake atakuwa anagawana nae majukumu ya nyumba kwa kiwango sawa, hali hiyo bado iko mbali kabisa.
Na katika upande wa familia ya rais, ? Veronica Carstens na mume wake rais wa Ujerumani Karl Castens hawakuwa na mtoto. Veronica Carstens alikuwa akimsindikiza mume wake kuanzia mwaka 1979 anapokwenda ziara za nje na katika matukio muhimu lakini pia alikuwa anaendesha shughuli zake za udaktari.
Mwandishi : Grunau, Andrea / ZR / Kitojo Sekione
Mhariri:Josephat Charo