1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Wakenya 200 wajiunga kupigana upande wa jeshi la Urusi

13 Novemba 2025

Serikali ya Kenya imesema zaidi ya raia wake 200 wamejiunga na jeshi la Urusi katika vita vinavyoendelea nchini Ukraine huku baadhi ya mashirika ya ajira yakiendelea kuwashawishi Wakenya zaidi kujiunga kwenye vita hivyo.

Ukraine | Chasiv Yar | Mwanajeshi wa Ukraine
Mwanajeshi wa Ukraine akijiandaa kufyatua kombora katika uwanja wa vita eneo la Chasiv YarPicha: Wojciech Grzedzinski/Anadolu/picture alliance

Katika taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje, Kenya imeeleza kuwa shughuli za kuajiri wapiganaji kwa ajili ya vita nchini Ukraine zimepanuka na sasa zinawalenga raia kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, wakiwemo Wakenya.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa zaidi ya Wakenya 200 tayari wamejiunga na jeshi la Urusi, na kwamba mitandao ya kuajiri wapiganaji hao bado inaendelea kufanya kazi ndani ya Kenya na Urusi.

Ubalozi wa Urusi mjini Nairobi haukujibu mara moja ombi la kutoa maoni kuhusu madai hayo.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, ubalozi wa Kenya mjini Moscow umerekodi visa vya Wakenya waliojeruhiwa ambao walishawishiwa kujiunga na vita kwa ahadi ya kulipwa kiasi cha dola 18,000 kufidia gharama za visa, usafiri na malazi.

Wiki iliyopita, Ukraine iliripoti kuwa zaidi ya raia 1,400 kutoka takriban nchi 30 za Afrika wanapigania upande wa Urusi, baadhi yao wakiwa wameajiriwa kwa njia za udanganyifu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW