1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Wakenya hawatoandikishwa kuipigania Urusi nchini Ukraine

16 Machi 2026

Serikali ya Kenya imesema imefikia makubaliano na Urusi ya kuzuia raia wa Kenya kuandikishwa kupigana katika vita vya Ukraine.

Kenya| Musalia Mudavadi
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia MudavadiPicha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi, amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa familia za Wakenya waliovutiwa kujiunga na jeshi la Urusi, kwa ahadi ya mishahara ya maelfu ya dola na bonasi kubwa.

Taarifa zinaonyesha kuwa zaidi ya Wakenya 1,000 wameajiriwa kupigana upande wa Urusi, idadi inayodaiwa kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyokadiriwa awali.

Akizungumza baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, mjini Moscow, Mudavadi amesema Wakenya hawataruhusiwa tena kuandikishwa kupitia Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Ameongeza kuwa huduma za kibalozi zitaimarishwa kusaidia Wakenya ambao tayari wamejiunga na vita hivyo.

Kwa upande wake, Lavrov amesema raia wa Kenya walisaini mikataba ya kupigana kwa hiari. Wakati huo huo, Ukraine inadai kuwa zaidi ya Waafrika 1,700 wanapigana upande wa Urusi katika vita hivyo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW