1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAKENYWA WATIA FORA KATIKA NEW YORK MARATHON

3 Novemba 2003

AFRIKA KUSI NI YAJIWINDA KWA CHANGAMOTO NA ALL-BLACKS (NEW ZEALAND) NA BAYER LEVERKUSEN IMEPOTEZA USUKANI WA BUNDESLIGA KWA STUTTGART

Bayer Leverkusen imepoteza jana usukani wa kuongoza Bundesliga kwa mudu suluhu 0:0 na Kaiserslauten. Leverkusen iliocheza finali ya Champions League mwaka jana imerudi nyuma nafasi ya pili ya ngazi ya Ligi ikiwa lakini pointi 1 tu nyuma ya VFB Stuttgart. Stuttgart ilinguruma kweli jumamosi mbele ya Freiburg kwa kuizaba mabao 4:1. Jana Borussia Dortmund ilitoka nyuma baada ya kuchapwa mabao 2 na Hamburg na kutia fora usoni na mwishoe kuondoka na ushindi wa mabao 3-2.Dortmund,mabingwa wa Ulaya wa 1997 sasa wmejongelea nafasi ya 4 kileleni mwa Bundesliga na kuwapiku mabingwa bayern Munich waliokiona kile kilichomtoa kanga manyoya katika changamoto yao ya kusisimua kati yao na schalke 04.Schalke iliizaba Munich mabao 2:0.

Kwa ushindi huo,Jupp Heynckes ameibuka juu ya timu yake ya zamani alieifunza na kuiongoza kutwaa ubingwa 1989 na 1990. Nje ya Bundesliga: Real Madrid,Deportivo la Coruna zote za Spain na Juventus ya Itali zinatarajia kukata na mapema tiketi zao za kuingia hatua ya kutoana ya champions League- Kombe la klabu bingwa barani Ulaya kati ya wiki hii: Real ikiania taji lake la 10 la Kombe la ulaya ndio inateremka mlima ikipambana wiki hii na Partizan Belgrade na kwa mara nyengine Real itawategemea mastadi wake akina Ronaldo na Luis Figo kutia mabao.

Kama Real, Juventus ya Itali inatazamia ushiundi wake 4 wa msimu huu wa Champions League,lakini watakua na changamoto kali mbele ya Real Sociedad ya Spain.Deportivo ina pointi 7 kileleni mwa kundi lake C na ushindi dhidi ya Monaco jumatano hii utaipatia La Coruna tiketi yake ya kujitosa katika duru za kutoana. Mabingwa wa ujerumani-Bayern Munich wakiwa kileleni mwa kundi AS lakini kwa pointi 1 kuliko Olympique Lyon ya Ufaransa inayocheza na mshambulizi wa zamani wa B.Munich Giovanne Elber,itabidi kukaba mbrazil huyo asitie bao atakapteremka tena katika Uwanja wa olimpik wa Munich.

Kura pia imepigwa kwa changamoto ya duru ya tatu ya Kombe la taifa la Ujerumani: Mapambano 3 yanazikumbanisha timu za daraja ya kwanza ya Bundesliga:Bayern Munich-mabingwa wanakumbana na washindi mara 3 wa Kombe hilo Hamburg.Stuttgart inayoongoza Bundesliga wakati huu imepangwa kupambana na Borussia Mönchengladbach na Werder Bremen watamalizana na Hertha Berlin.

Kutoka dimba tugeukie dimba la aina nyengine:Kombe la dunia la rugby linaloendelea sasa nchini Australia: Ushindi wazi wa Afrika kusini wa mabao 60-10 ya samoa katika mpambano wao uliopita umewaweka mabingwa hawa wa dunia wa 1995 katika mkondo barabara wa kuweza kunguruma tena,mradi watambe mbele ya All-Blacks-New Zealand katika changamoto yao ijayo ya robo-finali mjini Melbourne. Kocha wao Rudolf Straueli amesema kwamba timu yake imeboreka tangu pale iliposhindwa mabao 19-11 na New Zealand wakati wa mashindano ya mataifa 3 ya msimu wa mwaka huu.

Mchezo wa rugby wa Afrika kusini ulidhofika mno mapema mwaka huu kufuatia mlolongo wa matokeo yasio-ridhisha na ya kuvunja moyo ilipocheza na Ufaransa,Sscotland,New Zealand na Uingereza. Halafu kuliibuka mkasa wa ukabila pale mchezaji mashuhuri Geo Cronje kukataa kukaa chumba kimoja na mchezaji mrangi wa timu ya rugby ya Afrika kusini. Lakini ushuindi wa majuzi dhidi ya samoa,umenoa makucha ya timu ya rugby ya Afrika Kusini na sasa itayari kwa zahama nyengine na All-Blacks -New Zealand. Iwapo Afrika Kusini itatwaa tena Kombe la dunia la rugby kama 1995, ni swali la kusubiri na kuona.

NEW YORK-MARATHON: Wakenya wake kwa waume wametia tena fora katika mbio za New York marathon hiyo jana: Upande wa wanawake, Margaret Okayo alivunja rekodi yake mwenyewe kwa muda wa dakika 2 wakati upande wa wanaume, Marti n Lel alichukua muda wa masaa 2:24:21.Lel, mwenye umri wa miaka 24 na bingwa wa mbio za nusu-marathon wa dunia mwaka huu,alimshinda rafiki yake wa chanda na pete na bingwa wa mwaka jana Rodgers Rop pia kutoka Kenya.Mshindi wakike Okayo ambae hakutazamiwa kuwika kabla ya mbio hizi amepokea kitita cha dala laki 1 kwa ushindi wake na kitita kingine cha dala 60.000 kwa kuweka rekodi.Baada ya kumaliza mbio hizo Okayo aliomba dua kimya kimya na baadae akasema atachangia sehemu ya zawadi yake kuwasaidia watoto kwao Kenya ili wajipatie elimu bora. Mamlaka ya Kenya katika New York marathon yalibainishwa na kunyakua nafasi 4 za kwanza uoande wa wanaume-Martin lel -mshindi;Rodgers Rop wapili;Christopher Cheboiboch akamaliza watatu huku Mkenya mwengine Elly Rono akibidi kuridhika na nafasi ya 4. Upande wa wanawake nafasi ya kwanza na ya pili ilikwenda pia Kenya.Catherine Nderebaba alibidi kuridhika na nafasi ya pili akija nyuma ya mshindi Margaret Okayo. Wasichana wa Kenya sasa wameshinda mataji 5 ya mbio za New York marathon tangu 1994 na wenziwao wanaume wame pia mataji 5 tangu 1997.Okayo,ambae ameshinda kwa mara ya pili New York marathon,ni mshindi wa mwaka uliopita wa Boston marathon.


Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW