1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUganda

Kenya ilihusika na kukamatwa kwa Besigye asema wakili wake

Saleh Mwanamilongo
24 Novemba 2024

Wakili wa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye amesema kuna ushahidi wa ushiriki wa serikali ya Kenya katika kukamatwa na kutolewa kwa njia haramu kwa Besigye jijini Nairobi.

Wakili wa Besigye asisitiza Kenya ilihusika katika kutekwa kwake
Wakili wa Besigye asisitiza Kenya ilihusika katika kutekwa kwakePicha: BADRU KATUMBA/AFP

Kenya ilikana kuhusika, lakini wakili Erias Lukwago alidai serikali ya Kenya ilihusika. Alisema alipata nyaraka za Besigye licha ya upinzani kutoka idara za ujasusi za Kenya.

Msemaji wa serikali ya Uganda alidai operesheni hiyo ilifanyika kwa ufahamu wa Kenya.

Uganda imekuwa ikiendeleza ukandamizaji wa upinzani, ikiwemo kuwakamata wanachama 36 wa FDC nchini Kenya Julai mwaka huu.