1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi Afrika Magharibi, Kati wafikia milioni 14

20 Septemba 2024

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema idadi ya wakimbizi na watu waliolazimishwa kuyahama makaazi yao katika eneo la Afrika Magharibi na Kati imeongezeka maradufu tangu mwaka 2019.

Wakimbizi nchini Nigeria
Wakimbizi nchini NigeriaPicha: AUDU MARTE/AFP

Kamishna Mkuu wa UNHCR kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Abdouraouf Gnon-Konde, amewaambia waandishi habari mjini Abidjan kuwa idadi hiyo imepanda kutoka wakimbizi milioni 6.5 mwaka 2019 hadi milioni 13.7 mwaka huu.

Gnon-Konde alisema kufikia mwishoni mwa mwaka huu, idadi hiyo huenda ikaongezeka hadi kufikia kati ya watu milioni 14 na 15.

Soma zaidi: Afisa wa UN asema wanawake wakimbizi Sudan wanahitaji ulinzi

Hata hivyo, idadi hiyo haijumuishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako UNHCR inakadiria kuwa karibu watu milioni saba wamelazimika kuyahama makaazi yao.

Kutokana na kwamba watu wengi waliokimbia makaazi yao wanashindwa kurejea nyumbani kwa miongo kadhaa, UNHCR imezitaka nchi zinazowahifadhi kuwajumuisha wakimbizi katika mipango yao ya maendeleo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW