Kambi ya Dadaab inawahidahi wakimbizi takribani 350,000.
11 Mei 2018Serikali nchini Kenya, mara kadhaa imekuwa ikitangaza kuifunga kambi ya Dadaab iliyopo kaskazini mashariki mwa Kenya kwa sababu za kiusalama. Kambi hiyo ambayo kwa sasa inawakimbizi wapatao laki mbili na thelathini na tano elfu, inadaiwa kutokuwa na chakula cha kutosha kwa wakimbizi huku mashirika ya kimataifa yanayotoa misaada ya chakula yakionekana kuchoka kuendelea kutoa misaada hiyo hali inayoongeza hofu kwa wakimbizi.
Wakati anapitia kipindi cha maumivu yaliyosababishwa na kubakwa nchini Somalia, njaa ya mara kwa mara na kutokuwa na uhakika wa maisha yake katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya Fartun ni karibu sasa anasahau hisia za matumaini zikoje.
Miaka miwili iliyopita serikali ya Kenya ilisema kuwa ingeifunga kambi hiyo ya wakimbizi ambayo kwa muda huo ilikuwa ni kambi kubwa kabisa ya wakimbizi duniani. Serikali hiyo ilishindwa kufunga kambi ya Dadaab lakini kitisho kinaonekana juu ya wakazi wa eneo hilo.
Mwanzoni maisha kwa wakimbizi yalikuwa mazuri.
"Kabla ya hapo maisha katika kambi hiyo ya wakimbizi yalikuwa mazuri, lakini hayafanani." Alisema Fartun mwanamke mwenye umri wa miaka 37 na watoto 11.
Alirudi Somalia kama sehemu ya mpango maalumu wa wakimbizi kurejea nyumbani, alilaumiwa na kulazimishwa na vikundi vya haki za binadamu, lakini akarudi katika kambi ya Dadaab baada ya safari yake ya kurudi nyumbani kumwendea vibaya. Ilikuwa ni tarehe 16 mwezi Mei mwaka 2016 wakati kila kitu kilibadilka katika maisha ya Fartun.
Kenya ilitangaza kuifunga kambi ya Daadab iliyokuwa na watu takribani 350,000, nakusema kuwa wakimbizi watarudishwa katika nchi zao.
Bila kuwa na ushahidi, serikali ya Kenya pia ilidai kuwa Dadaab ilikuwa ni msingi wa mashambulizi ya ugaidi nchini humo yaliyofanywa ka kundi la Al-Qaeda, kwa kushirikiana na kundi lingine la kigaidi la Al-shabaab. "Serikali ya Kenya iliwahi kusema kuwa itaifunga kambi hiyo, lakini tamko la wakati huu ni tofauti inaonekana lina msisitizo na limekusudiwa". Alisema Fartun.
Kwa kupuuza wasiwasi wa mashirika ya misaada ya kimataifa, tarehe ya mwisho Novemba 2016 ilianzishwa hapo awali, na kisha ikaahirishwa hadi mwaka wa 2017, ilikuwa ni programu ya miaka miwili iliyoitwa "uhamisho wa kujitolea" .
Wakati akizungumza na shirika la habari la AFP Fartun alisema kuwa katika kambi ya Dadaab taarifa zilienea kuwa kama wakimbizi hawataondoka basi watapigwa, ingawa amekiri kuwa taarifa hizo sio za uhakika. Fartun alirudi Somalia mwezi june mwaka 2016, akiwa pamoja na familia yake.
Fartun anakumbuka kipindi cha mateso yanayoambatana na kubakwa.
Lakini mwendo wa kilometa kama tano ndani ya Somalia Fartun na familia yake walivamiwa na wanaume wenye silaha na wakachukuliwa mateka. Fartun anasema alibakwa mara kadhaa kabla ya kuachiwa huru. Kijana wake mkubwa mwenye umri wa miaka 12 Abdirizak alichukuliwa ili aingizwe katika kundi la wanamgambo.
Hatimaye Abdirizak na mama yake walikutana tena miezi michache baadae , baada ya kijana huyo kufanikiwa kutoroka katika kundi la wanamgambo na baadae wote wakarudi katika kambi ya Dadaab .
Kurudi katika kambi hiyo lilikuwa ni jambo gumu kwa Fartun ambaye alibaini kuwa mambo mengi yamebadilika na kuwa mabaya zaidi.
Fatuma amesema tangu waliporudi wamekuta hakuna chakula cha kutosha, na wanaishi katika nyumba ya ndugu wa wifi yake kwa sababu hawana nyumba nyumba yao.
Mwandishi: Veronica Natalis/ AFP
Mhariri: Gakuba, Daniel