1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi nchini Burundi waanza maisha mapya kama Watanzania.

17 Juni 2010

Maisha ya wakimbizi waliorudi nchini Burundi yangali duni.

Wakaazi wa Bujumbura.Picha: AP

Miongoni mwa wakimbizi milioni moja walioikimbia nchi ya Burundi kutokana na vita vya muda wa miaka 40 ,baadhi wanaanza maisha mpaya kama Watanzania huku wale walioamua kurudi  hadhi yao katika shirika la Umoja wa mataifa imegeuka kutoka wakimbizi hadi kuwa watu waliochwa bila makaazi.

Wakati  shirika la umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi likitangaza kiwango kidogo zaidi duniani  cha kurudi makwao wakimbizi kuwa kushuhudiwa  katikamuda wa miongo miwili ,visa  vinavyothibitisha jinsi ilivyo vigumu kwa wakimbizi kurudi makwao ni vile vya nchi hiyo ya Burundi.

Kwa maelfu ya wakimbizi wa Burundi walioikimbilia nchi jirani ya Tanzania katika miaka ya 70,baada ya miongo minne sasa wamekuwa raia wa Tanzania.

Hii ni baada ya hatua iliyotangazwa  na serikali ya Tanzania  mwezi Aprili mwaka huu kuwahalalisha Warundi takriban 162,000 na familia zao kuwa Watanzania.

Wengi wa wakimbizi hao waliokuwa wakiishi katika kambi tatu kubwa magharibi mwa  Tanzania walikuwa wamekosa matumaini ya kuwa raia na kudhani kuwa wengi wao wangekufa wakiwa bado wakimbizi.

Wiki chache zilizopita, Ferederiko Kivulunzi mwenye umri wa miaka 59 ana ambaye aliwasili Tanzania akiwa na miaka 21 1972 alipoyakimbia machafuko kwao Burundi anasema" sasa wameondokana na  ile hali ya kuitwa wakimbizi na kuweza kujivuna kwamba sasa ni Watanzania. Anasema sasa wanaweza kutembea  wakiwa huru kama Mtanzania mwengine yeyote."

Sasa furaha inaonekana miongoni mwao kufuatia uamuzi huo ambao pia unawaruhusu kuzunguka huru  kinyume na ilivyokuwa walipokuwa kambini kama wakimbizi.

Hata hivyo hali ni tofauti nchini Burundi ambapo maisha ya wakimbizi takriban nusu milioni walioamua kurudi nchini humo yangali duni.

Nyumba mojawapo kwa wakimbizi wa Burundi wanaorudi nyumbani.Picha: picture-alliance/ dpa

wengi wao wanakosa ardhi za kuishi,baada ya ardhi zao kunyakuliwa na waliokuwa majirani zao ama kutokana na miradi iliyoanzishwa na  serikali katika ardhi hizo.

Wengi wa wakimbizi hawa wameamua kupata hifadhi katika kijiji kimoja kinachofahamika kama 'kijiji cha amani'kilicho jengwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi kwa minajili ya kuwahifadhi maelfu ya Wahutu wanaorudi nchni humo na Watutsi walioachwa bila makaazi  nchini humo ambao serikali haijui iwafanyeje.

Sambamba na  nyumba ndogo, wanaorudi n yumbani hupewa mbuzi watatu na mipapai na mipera iliokwisha oteshawa. Mkimbizi mmoja kawa jina la Saphia anaishi mtaa watatu  wa  wa eneo hilo la makaazi, nyumba nambari 125, anasema anashukuru kwa kupatiwa nyumba lakini analalamika kwamba waliorudi nyumbani na kupewa makaazi katika kijiji hicho cha amani hawana njia ya  kukidhi mahitaji yao kimaisha kwa sababu hawana ardhi. Wote wanategemea vibarua vya kubahatisha ambapo malipo ya kazi ni mabaya mno.

Naye Densis Niyungeko anayeishi nyumba  nambari 238 katika mtaa wa sita, alizaliwa Congo iliokuwa zamani Zaire baada ya wazazi wake Warundi kukimbilia huko 1972.   Yeye pia aakaikimbia Congo wakati wa vita vya 1996-97 kwanza akikimbilia Tanzania na baadae kurudi nymbani kwa asili  Burundi. na ingawa hufafadhahika baadhi ya wakati kwa ukosefu wa ajira  ya kudumu na kutegemea kibarua cha reja reja, hata hivyo anasema anafuraha kurudi nyumbani. aanamalizia kwa usemi, uhamishoni ni uhamishoni tu- mtu Kwao !

Mwandishi: Maryam Dodo Abdalla/AFP

Mhariri:Abdul-Rahman,Mohammed

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW