Italia inakabiliwa na mzigo mzito kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi na inawapeleka katika mataifa mengine bila kuwasajili. Kwa njia hiyo maelfu ya wakimbizi wako njiani katika nchi za Ulaya - bila kusajiliwa kama wakimbizi. Wengi wanataka kuingia Uingereza lakini nchi hiyo inaifunga mipaka yake.