1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Wakorea Kusini waandamana kwenye makazi ya Yoon Suk Yeol

5 Januari 2025

Maelfu ya raia wa Korea Kusini wameandamana leo Jumapili ili kumuunga mkono au kumpinga Rais Yoon Suk Yeol, aliyesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kwa jaribio lake la kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi.

 Seoul 2025 | Maandamano I Yoon
Maelfu ya raia wa Korea Kusini wakiwa kwenye maandamano kwenye makazi ya Rais YoonPicha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Maelfu ya raia wa Korea Kusini wameandamana leo Jumapili ili kumuunga mkono au kumpinga Rais Yoon Suk Yeol, aliyesimamishwa kazi kutokana na kushindwa kwa jaribio lake la kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi na kupinga kukamatwa siku moja kabla ya muda wa waranti ya kukamatwa kwake kumalizika.

Yoon aliiingiza nchi hiyo katika machafuko ya kisiasa mwezi uliopita kwa tamko la kuanzisha sheria ya kijeshi na tangu wakati huo amejificha katika makazi ya rais, akizungukwa na mamia ya maafisa wa usalama wanaomtii.

Soma pia: Maelfu ya waandamanaji Korea Kusini wakusanyika Seoult

Siku ya Ijumaa, vikosi vya wachunguzi vilishindwa kumkamata rais Yoon baada ya mvutano mkali uliodumu kwa muda wa saa sita kati ya idara yake ya usalama, huku wafuasi wake pia wakipiga kambi nje ya makazi yake.

Jumapili hii, Maelfu ya watu wamefika kwenye makazi yake tena licha ya baridi kali na theluji, kambi moja ikitaka Yoon akamatwe huku nyingine ikitaka kushtakiwa kwake kutangazwe kuwa ni batili.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW