1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakosoaji wa serikali wakamatwa Tunisia

14 Februari 2023

Mamlaka ya Tunisia imemkamata kiongozi wa chama cha upinzani cha Ennahda, katika kamata ya wapinzani wake wakiwemo wanasiasa na wakosoaji wa rais anayeongoza kimabavu, Kais Saied.

Tunesien Tunis | Protest gegen Kais Saied
Picha: FETHI BELAID/AFP

Kulingana na wakili wa vuguvugu hilo, Ines Harrathi, kiongozi wa Ennahda Noureddine Bhiri, alikamatwa nyumbani kwake mjini Tunis kwa madai ya kuwa sehemu ya njama ya kuvuruga usalama wa taifa. 

Lazhar Akremi,  wakili na mkosoaji mkubwa wa rais Saied na Noureddine Bouttar mkurugenzi wa chombo cha habari kinachojisimamia cha Mosaique,  pia walikamatwa na maafisa wa polisi usiku wa kuamkia leo.

Soma pia:Mwanaharakati wa Tunisia Khayam Turki akamatwa na polisi

Hadi sasa serikali haijatoa tamko lolote juu ya kamata kamata hiyo iliyoanza mwanzoni mwa juma hili. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW