Mageuzi ya Togo yanaacha nafasi ndogo ya mabadiliko
24 Aprili 2024Ingawa vyama vinaendelea kufanya kampeni, matumaini ya mabadiliko ya kisiasa katika uchaguzi wa Aprili 29, ulioahirishwa mara kadhaa na serikali, ni finyu.
Jean Yaovi Degli, mwanasheria na waziri wa zamani wa uhusiano wa bunge, amesema hawapaswi kuwa na matarajio mengi katika uchaguzi ujao, akidai kwamba chama tawala hakiogopi chochote.
Togo yasogeza mbele uchaguzi wa bunge
Wabunge siku ya Ijumaa waliidhinisha mageuzi ya kubadili mfumo wa urais hadi wa bunge ambao vyama vya upinzani vinasema utamruhusu Rais Faure Gnassingbe kurefusha mamlaka yake.
Chini ya mfumo huo mpya, wabunge, badala ya wananchi, watamchagua rais ambaye atahudumu kwa miaka minne. Aidha madaraka yatahamia kwa wadhifa mpya wa rais wa baraza la mawaziri, aina ya jukumu la waziri mkuu, ambaye atakuwa kiongozi wa chama cha walio wengi katika bunge.