Wakulima kuandamana dhidi ya rais Macron
24 Februari 2024Matangazo
Wakulima wanajiandaa kuandama leo dhidi ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati atakapoyatembelea maonesho makubwa ya kilimo mjini Paris, huku kukiwa na ghadhabu kuhusu gharama na sheria za kuyalinda mazingira.
Wakulima wamekuwa wakiandamana kote barani Ulaya wakitaka mapato bora na urasimu upunguzwe na wanalalamika kuhusu ushindani usio wa haki kutoka kwa bidhaa za bei nafuu kutoka nchini Ukraine.
Mwaka 2022 Umoja wa Ulaya uliondoa ushuru wa uagizaji wa chakula kutoka Ukraine kuisaidia nchi hiyo kiuchumi kufuatia uvamizi wa Urusi. Maonesho ya kilimo ya mjini Paris ni tukio kubwa nchini Ufaransa linalowavutia wageni takriban 600,000 katika kipindi cha siku tisa.