Wakulima Ubelgiji kufunga njia za bandari ya Zeebrugge
30 Januari 2024Matangazo
Gazeti la kila siku la De Tijd limeripoti kuwa wakulima hao wanalenga kuzuia kufukiwa bandari hiyo iliyo ya pili kwa ukubwa nchini Ubelgiji kwa muda wa saa 36 zinazokuja.
Polisi imesema imeuarifu uongozi wa bandari ya Zeebrugge kuhusu mipango hiyo ya wakulima ambao wamekusanya mamia ya matrekta na malori kwa dhima ya kuzifunga barabara.
Soma pia:Wakulima waandamana nchini Ufaransa kuishinikiza serikali itazame hatma ya sekta hiyo
Hatua hiyo itaendelea licha ya tangazo kuwa- waziri mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo anapanga kukutana na vyama vya wakulima leo Jumanne.
Maandamano hayo yanafuatia mengine yaliyofanywa na wakulima karibu kote barani Ulaya ikiwemo nchini Ujerumani, Poland, Ufaransa na Romania.