1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Utawala wa sheria

Wakulima wapunguza shehena za kahawa kuingia Ulaya

27 Desemba 2023

Waingizaji kahawa kwenye mataifa ya Umoja wa Ulaya wameanza kupunguza shehena wanazoagiza kutoka kwa wakulima wadogo barani Afrika na maeneo mengine duniani. Hatua hiyo ni maandalizi ya utekelezeaji wa sheria mpya.

Kilimo | Mkulima akionesha zao la kahawa shambani
Mkulima akionesha zao la kahawa likiwa shambaniPicha: Ute Grabowsky/photothek/picture alliance

Hatua hiyo ni maandalizi ya utekelezeaji wa sheria mpya ya umoja huu inayopiga marufuku manunuzi ya bidhaa zilizozalishwa kwa kuharibu misitu, jambo linalochangia mabadiliko ya tabianchi. Utekelezaji wa sheria hiyo unatishia ustawi wa mamilioni ya wakulima wanaotegemea soko la Ulaya kuuza mazao yao.

Duru kutoka na ndani ya viwanda na makampuni yaliyo ndani ya Umoja wa Ulaya ambayo huaagiza kutoka mazao mfano wa kahawa zinasema utekelezaji wa matakwa ya sheria hiyo mpya utabadili kabisa hali ya soko la mazao na bidhaa nyingine duniani.

Sheria hiyo yenye dhamira ya kupambana na uharibifu misuti itaanza kufanya kazi mwishoni mwa mwaka ujao wa 2024. Hata hivyo makampuni tayari yameanza kuchukua hatua za mapema yakiohofia ukiukaji wa masharti yake.

Inaarifiwa kampuni kubwa nne tayari zimepunguza uagizaji kahawa kutoka nchini Ethiopia, taifa ambalo kaya karibu milioni 5 zinategemea zao hilo kiuchumi.

Soma pia:Mkutano wa kimataifa kuhusu mustakabali wa misitu ya kitropiki unaendelea Kongo

Kampuni hizo zimetoa hadhari kwamba mikakati wanayolazimika kuichukua kujiepusha na kukiuka sheria inayokuja inatishia kuwatumbukiza mamilioni ya wakulima kwenye umasikini, kupandisha bei za bidhaa kwa walaji barani Ulaya na hata kuvuruga malengo ya Umoja wa Ulaya ya uhifadhi wa misitu.

 "Sioni uwezekano wa kununua kiwango kikubwa cha kahawa ya Ethiopia kuanzia sasa na kuendelea" amesema Johannes Dengler, mkuu wa kampuni ya kusindika kahawa ya Dallmayr, ambayo inanunua kiasi asilimia moja ya kahawa yote duniani.

Matakwa ya sheria katika kulinda misitu

Chini ya sheria mpya la ulinzi wa misitu ya Umoja wa Ulaya waagizaji bidhaa kama kahawa, kokoa, soya, chikichi, mbao, mpira na mifugo watapaswa kuthibitisha kuwa bidhaa zao hazitokani na uzalishaji uliofanyika kwenye ardhi ambayo kabla ilikuwa misitu. Iwapo watashindwa kufany ahivyo watakabiliwa na kikwango kikubwa cha faini.

Mwanamke akianika kahawa nchini KenyaPicha: Ute Grabowsky/photothek/picture alliance

Kampuni kubwa ya kutengeneza kahawa ya JDE Peets imesema italazimika kuwaondoa wakulima wadogo kutoka miongoni mwa wasambazaji wake iwapo hadi mwezi Machi mwakani watashindwa kukubailiana jinsi ya kutekeleza masharti ya sheria mpya.

Uharibifu misitu ni sababu ya pili ya inayochangia janga la mabadiliko ya tabianchi ukiyaweka kando matumizi ya nishati za visukuku.

Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imesema inayo mikakati kadhaa ya kuzisaidia nchi duniani na wakulima wadogo kutimiza masharti y sheria hiyo mpya.

Miongoni mwa mikakati hiyo ni kupitia mfuko ulizinduliwa wakati wa mkutani wa kimataifa wa amzingira wa COP28 ambao Umoja wa Ulaya na nchi wanachama zimeahdi kuchangia dola millioni 76.

Soma pia:Dunia 'imeshindwa' kutimiza ahadi ya kukomesha ukataji miti ifikapo 2030

Sheria hiyo mpya inayataka makampuni kufanya tathmini kwa njia za kidijitali kubaini wapi zilikotoka malighafi na ardhi iliyotumika kuzikuza. Hilo litazilazimisha kampuni kuyafuatilia moja kwa moja mamilioni ya mashamba madogo madogo kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi.

Hata hivyo kwa sababu makampuni makubwa yanategemea zaidi madalali kupata bidhaa kutoka kwa wakulima, hayawezi kuwategemea watu hao kupata taarifa za uhakika kuhusu maeneo mazao yalikozalishwa kwa hofu ya kutokuwepo uaminifu au madalali hao nao vilevile hutumia mawakala badala ya kufika mashambani.

Kuna suala la kukosekana njia imara za mawasiliano ya simu na hata intaneti kwenye maeneo ya vijiji kuliko namashamba madogo madogo. Kuna migongano ya maslahi, migogoro ya ardhi na hata wakulima kutokuwa na elimu ya kutosha, changamoto zote hizo kwa jumla zitaifanya kazi ya kukusanya taarifa na kutunza takwimu kuwa ngumu.

Mwelekeo wa makampuni  katika kutekeleza sheria

Kwenye baadhi ya mazao kama Kahawa makampuni yataona bora kuhamia kwa wazalishaji wakubwa wenye uwezo wa miundombinu na kifedha kukusanya takwimu zinazohitajika chini ya matakwa ya sheria mpya. Hivi sasa tayari abadhi ya kampuni zinawekeza nguvu za uagizaji kahawa kutoka kwa mabwenyenye huko Brazil na kuwapa kisogo wakulima wadogo.

Hata hivyo kuachana kabisa na wakulima wadogo au kuachana kabisa na nchi zinazozalisha kwa wingi baadhi ya mazao siyo jambo linaloweza kutekelezwa kikamilifu.

Juhudi za kuzuwia kupotea kwa misitu asilia ya Kongo

02:44

This browser does not support the video element.

Mathalani Ivory Coast na Ghana zinazalisha asilimia 70 ya kakao yote duniani, huku asilimia 60 ya kahawaduniani inatoka Brazil na Vietnam. Indonesia na Malaysia zinawakilisha asilimia 90 ya mafuta yote ya chikichi yanayotumika duniani.

Soma pia:Idadi ya wanyama pori ulimwenguni kote yapungua kwa 69%

Kutokana na ukweli huo makampuni barani Ulaya yameashiria yatalazimika kupeleka bidhaa wasizoweza kupata takwimu za uzalishaji wake kwenye masoko nje ya Umoja wa Ulaya. Iwapo mkakati huo ndiyo utatumiwa na kampuni nyingi utafubaza malengo ya Umoja wa Ulaya ya kuilinda misitu.

Hiyo ni kwa sababu bidhaa bado zitaendelea kuzalishwa kutona na malighali zilizolimwa kwenye ardhi ambayo kabla ilikuwa misitu lakini tofauti yake ni kwamba hazitouzwa ndani ya Umoja wa Ulaya. Na kampuni nyingi huo ni ukweli usifichika.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW