1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKimataifa

Wakuu wa mashirika ya fedha kujadili maendeleo ya kimataifa

21 Oktoba 2024

Wakuu wa mashirika ya fedha duniani watakusanyika mjini Washington Marekani wiki hii huku kukiwa na wasiwasi mkubwa juu ya vita katika Mashariki ya Kati na Ulaya, uchumi wa China unaodorora.

Mkutano wa Marrakesh wa IMF na Benki ya Dunia 2023
Mkutano wa Marrakesh wa IMF na Benki ya Dunia 2023Picha: Mosa'ab Elshamy/AP

Mikutano ya kila mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF na Benki ya Dunia inatarajiwa kuwavutia zaidi ya watu 10,000 kutoka wizara za fedha, benki kuu na makundi ya asasi za kiraia kujadili juhudi za kuimarisha maendeleo ya kimataifa, kushughulikia tatizo la madeni na kufadhili mchakato wa matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira.

Soma: IMF yaidhinisha mageuzi ya kupunguza gharama za kukopa kwa asilimia 36

Lakini changamoto kubwa katika mikutano hiyo itakuwa uwezekano wa ushindi wa uchaguzi wa Novemba 5 wa mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump katika kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa uchumi wa kimataifa kwa ushuru mkubwa mpya wa marekani na ukopeshaji, pamoja na kujiondoa katika ushirikiano wa hali ya hewa.

Josh Lipsky, afisa wa zamani wa IMF ambaye kwasasa anaongoza kituo cha Baraza la Atlantiki la Jiografia na uchumi, amesema kuwa suala muhimu zaidi kwa uchumi wa dunia ambalo ni matokeo ya uchaguzi wa Marekani, haliko kwenye ajenda rasmi wiki hii lakini liko katika mawazo ya kila mtu.Viongozi wa ulimwengu wasisitiza uwekezaji katika Nishati Jadidifu

Washiriki wa mkutano wa mwaka 2023 wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia huko Marrakesh Picha: Fadel Senna/AFP

Lipsky ameongeza kuwa uchaguzi huo una athari kubwa kwa sera ya biashara, hasa kuhusu mustakabali wa dola na mwenyekiti mpya wa benki kuu ya Marekani na kwamba yote hayo yanaathiri kila nchi duniani.

Naibu wa Rais wa Marekani Kamala Harris, ambaye ni mgombea urais wa chama cha Democratic, anatarajiwa pakubwa kuendelea na kuanzishwa tena kwa ushirikiano wa kimataifa na utawala wa Biden katika masuala ya hali ya hewa, kodi na msamaha wa madeni ikiwa atashinda katika uchaguzi wa mwezi ujao.Kenya yashuka zaidi katika nchi zisizoweza kukopesheka

Mikutano hiyo iliyoanza jana Jumatatu, na inayotarajiwa kupamba moto baadaye wiki hii, huenda ikawa ya mwisho kwa waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen, ambaye aliongoza kwa kiasi kikubwa juhudi za kimataifa za uchumi na hali ya hewa za utawala wa Rais Joe biden.

Yellen amesema huenda atamaliza kuhudumu katika utumishi wa umma baada ya kukamilika kwa muhula wa uongozi wa Rais Biden mwezi Januari.Benki ya Dunia yazindua mpango wa kusitisha kwa muda malipo ya madeni kwa nchi zilizokumbwa na maafa

Lakini kuongezeka kwa kauli dhidi ya biashara za China na mipango ya sera za viwanda kutoka kwa nchi tajiri kulikotiliwa chumvi na hatua ya utawala wa Rais Biden ya kuongeza ushuru kwa magari ya umeme ya China , pamoja na bidhaa zinazotumia umeme unaotokana na nguvu za jua, kunatarajiwa kuwa mada muhimu katika mikutano hiyo.

IMF itaelezea utabiri wa ukuaji wake wa kimataifa hii leo Jumanne.

Wiki iliyopita, mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva, alisema kuwa dunia iliyojaa madeni makubwa, inaelekea katika ukuaji wa pole pole na kuashiria siku za baadaye zenye changamoto.Hizi ndizo nchi zenye ufisadi mdogo zaidi duniani

Wanaharakati wakiandamana katika mkutano wa Marrakesh Picha: Fadel Senna/AFP

Huku kiwango cha kutolipa madeni miongoni mwa nchi maskini kikiwa huenda kimefikia kilele, washiriki katika mikutano hiyo ya kila mwaka wanatarajiwa kujadili ongezeka la tatizo la ukosefu wa fedha ambalo linayalazimu baadhi ya masoko yanayoibuka na yanayokumbwa na gharama kubwa za malipo ya madeni kuchelewesha uwekezaji wa maendeleo huku misaada ya kutoka nje ya nchi hizo ikipungua.

Mikutano ya mwaka jana ya IMF na Benki ya Dunia ilifanyika huko Morocco huku kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas likiishambulia Israel, na kuua zaidi ya watu 1,200 na pia kusababisha migogoro na vifo vya zaidi ya raia 40,000 wa Gaza, haya ikiwa ni kulingana na mamlaka ya afya ya Palestina.

Uharibifu wa kiuchumi unaonekana kuathiri pakubwa chumi zilizo ndani ama karibu na mzozo huo: Gaza, Ukingo wa Magharibi, Israel, Lebanon, Misri na Jordan.Migawanyiko ndani IMF, Benki ya Dunia kuhusu vita vya Gaza

Msaada kwa ajili ya Ukraine pia utakuwa mada kuu katika mikutano hiyo, kwasababu nchi tajiri za G7 zinalenga kufikia makubaliano ya kisiasa kufikia mwisho wa Oktoba kwa ajili ya mkopo wa $50 bilioni kwa Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW