1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakuu wa nchi EAC wachagua Katibu Mkuu mpya wa jumuiya

Veronica Natalis
7 Juni 2024

Mkutano wa kilele wa 23 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, umemuidhinisha Veronica Mueni Nduva raia wa Kenya, kuwa katibu mkuu mpya wa Jumuiya hiyo, auchukua nafasi ya Dr. Peter Mathuki.

Baadhi ya Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Baadhi ya Wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika MasharikiPicha: Presidential Press Unit Uganda

Dr. Peter Mathuki alichaguliwa na nchi yake  yake kuwa Balozi wa Kenya nchini Urusi.

Kuchaguliwa kulitanguliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kusababisha upotevu wa fedha za zaidi ya dola miliomi sita za Marekani. 
 
“Mimi Veronica  Mueni Nduva katibu mkuu mteule wa Jumuiya ya Afrika mashariki, ninaapa kuwa mwaminifu na muadilifu katika majukumu niliyopangiwa, hasa kusimamia mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na kuendesha majukumu yangu kwa maslahi ya Jumuiya. Sitashawishika kupokea maagizo yeyote kutoka nchi wanachama yaliyokinyume na mkataba na ambayo hayana maslahi ya wanajumuiya. Mungu nisaidie.” 

Soma pia:EAC yataka suluhu ya mzozo wa Kongo kwa njia ya mazungumzo
 
Veronica Nduva Raia wa Kenya, alitamka maneno hayo wakati akila kiapo cha utumishi katika mkutano huo wa wakuu wan chi, uliofanyika Juba Sudan kusini na kurushwa kwa njia ya mtandao.

Veronica Nduva anaandika historia ya kuwa mwananke wa Kwanza kuwa katibu mkuu wa Jumuiya hiyo kongwe barani Afrika, ambaye kabla ya uteuzi huu, alikuwa akihudumu kama Katibu Mkuu wa idara ya utendaji na usimamizi wa katika katika wizara ya huduma za umma, ambaye anauzoefu mkubwa katika masuala yay a utawala na usimamizi wa umma.  

Kuteuliwa kwa Katibu Mkuu

Uteuzi wa Nduva hata hivyo ulifanyika baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wa Caroline Mwende Mueke ambaye alibadilishwa kutokana na sababu za kisiasa.

Rais wa Kenya William Ruto wakati akizungumza katika mkutano huo amemtakia utumishi mwema Katibu mkuu huyo mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
“Jamhuri ya Kenya ilimteua Veronica Ndua kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kushika nafasi ya Dr. Peter Mathuki, ambaye pia tunamtakia majukumu mema ya ubalozi huko Urusi." Alisema rais Ruto.

Aliongeza kuwa "Kenya inaahidi kuendelea kufuatilia na kutoa ushirikiano wa shughuli na miradi yote ya Jumuiya kwa manufaa ya wanaafrika Mashariki.”

Soma pia:Samia, Museveni na Ruto wakutana kujadili EAC na Uchumi
 
Kikao cha Marais bado kinaendelea ambapo pia kitazingatia uidhinishwa kwa wa jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki kutoka jamhuri ya Kenya, Jaji wa Mahakama ya Rufani wa Tanzania Omar Othuman Makungu, aliyeteuliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki Diviseni ya Rufani katika mkutano wa marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mei mwaka 2023 mjini Bujumbura, Burundi. 
 
Mkutano huo umehudhuriwa na marais sita wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku Burundi ikituma mwakilishi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW