Wakuu wa vyama vya wafanyakazi watiwa mbaroni nchini ZImbabwe
13 Septemba 2006Polisi nchini Zimbabwe wamewakamata wakuu wa vyama vya wafanyakazi,wamezifunga njia ,wameuzingira uwanja mkuu mjini Harare pamoja na kuwatimua wanaharakati wanaoandama kupinga umasikini na kuipinga serikali pia ya rais Robert Mugabe.Msemaji wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi MLAMLELI SIBANDA amesema viongozi 15 wa vyama vya wafanyakazi na wanaharakati wamekamatwa Harare , wengine 20 wamekamatwa Bulawayo na wanne wengine katika mji wa kaskazini magharibi wa Chinhoyi.Miongoni mwa waliokamatwa ni mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi LOVEMORE MATOMBO na katibu mkuu Wellington Chibebe..Akizungumza kwa simu na kituo cha matangazo cha BBC,bwana Chibebe amesema polisi wamewapiga kwa marungu.Chama kikuu cha wafanyakazi kilichokua pia kiitishe maandamano hii leo,kinasemekana kimeamua kutoitisha maandamano hayo.