1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Walinda amani 4 wa UN wajeruhiwa kusini mwa Lebanon

Sylvia Mwehozi
30 Machi 2024

Umoja wa Mataifa umedai kuwa waangalizi wake wanne wa kijeshi wamejeruhiwa leo Jumamosi, wakati bomu lilipolipuka karibu nao, kusini mwa Lebanon.

Kikosi cha UNIFIL
Kikosi cha UNIFIL nchini LebanonPicha: Ariel Schalit/AP Photo/picture alliance

Umoja wa Mataifa umedai kuwa waangalizi wake wanne wa kijeshi wamejeruhiwa leo Jumamosi, wakati bomu lilipolipuka karibu nao, kusini mwa Lebanon.Makabiliano yaongezeka mpakani mwa Israel-Lebanon

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia mapatano UNTSO halikutaja chanzo cha mlipuko huo, ingawa shirika la habari la Lebanon limeishutumu Israel.

Taarifa ya shirika hilo imesema vitendo vya kuwalenga walinda amani havikubaliki na kutoa wito kwa pande zote kuzingatia sheria za kimataifa za kujizuia kuwashambulia watu wasio wanajeshi, wakiwemo walinda amani, waandishi wa habari, maafisa wa matibabu na raia. Mjumbe wa Marekani aonya dhidi ya vita mpakani mwa Lebanon

Israel imekuwa ikishambuliana karibu kila siku na wapiganaji wa vuguvugu la Hezbollah nchini Lebanon, wanaoungwa mkono na Iran tangu vita na kundi la wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza vilipoanza Oktoba 7.