1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Walinda amani 8 wa UN wakamatwa Kongo kwa utovu wa nidhamu

12 Oktoba 2023

Ujumbe wa MONUSCO, wametangaza kuchukuwa hatua kali dhidi ya wanajeshi wake wanaotuhumiwa kwa makosa makubwa.

Baadhi ya walinda amani wa MONUSCO nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikamatwa au kusimamishwa kazi kwa tuhuma za unyanyasaji kingono na mashambulizi.
Baadhi ya walinda amani wa MONUSCO nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikamatwa au kusimamishwa kazi kwa tuhuma za unyanyasaji kingono na mashambulizi.Picha: Djaffar Sabiti/REUTERS

Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUSCO, kimetangaza kuchukuwa hatua kali dhidi ya wanajeshi wake wanaotuhumiwa kwa makosa makubwa.

Kwa mujibu wa nyaraka za ndani zilizoonekana na shirika la habari la AFP, walinda amani wanane waliokuwa mjini Beni, mashariki mwa Kongo, walikamatwa tarehe Mosi Oktoba, na mmoja alisimamishwa kazi wiki moja baadaye kwa tuhuma za unyanyasaji kingono na mashambulizi.

Wote tisa ni wanajeshi kutoka Afrika Kusini na huenda wakawa wanahusika na kile nyaraka hizo zinachokiita "uvunjaji ulioenea wa kanuni za Umoja wa Mataifa." 

Taarifa iliyotolewa jana na MONUSCO imesema tayari maafisa hao wanaanza kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sera ya kutokuvumilia utovu wa nidhamu ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW