1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kuwarejesha nyumbani walinda amani 9 kwa unyayasaji DRC

14 Oktoba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa limesema litawarejesha makwao walinda amani tisa wa Afrika ya Kusini wanaotuhumiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia na wa aina nyingine mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

DR Kongo | MONUSCO | Unrühen
Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Umoja huo umesema umeamua kuchukua hatua hiyo kutokana na uzito wa tuhuma dhidi ya wanajeshi hao. Afisa wa ngazi ya juu kati ya hao anatuhumiwa kujaribu kukwamisha uchunguzi wa madai hayo na kuwatishia walinda amani wengine.

Soma zaidi: MONUSCO yazindua kampeni dhidi ya unyanyasaji wa kingono

Kulingana na taarifa ya Umoja wa Mataifa, maafisa wengine wa ngazi ya juu wanaokabiliwa na mashtaka, wataondolewa kwenye nafasi zao na kuongeza kuwa, tathmini ya awali imegundua kuwa walinda amani tisa walikuwa wakijihusisha na mahusiano kinyume cha maadili wakati wa muda wa marufuku ya kutokutoka nje, katika baa ambazo vitendo vya kikahaba vinafanyika.

Soma zaidi: Umoja wa Mataifa hatiani kuhusu unyanyasaji wa kingono DRC

Wanajeshi hao wanatuhumiwa pia kuwa waliwashambulia wafanyakazi wengine wa ujumbe wa kulinda amani na askari polisi waliokuwa wakijaribu kuwakamata. Umoja wa Mataifa umeahidi kuwa utawasaidia waathiriwa wa vitendo hivyo vilivyofanywa na maafisa wake

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW