1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Walinda amani wa umoja wa Mataifa waondoka Mali

17 Oktoba 2023

Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Mali vimetangaza kuanza kujiondoa kutoka kwenye kambi zao mbili za Tessalit na Aguelhok katika eneo lenye mvutano la Kidal.

Bundeswehr in Mali
Nembo ya kikosi cha jeshi cha Umoja wa Mataifa MINUSMAPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Hatua inayoibua hofu kwamba mapigano yatazidi kati ya wanajeshi na wapiganaji wenye silaha. 

Vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, MINUSMAvilitarajiwa kuondoka katika kambi zake katikati ya mwezi Oktoba lakini vikaahirisha wakati eneo hilo lililopokabiliwa na ongezeko la machafuko ya kupigania udhibiti wa maeneo.

Soma pia:Waasi nchini Mali wadai kudhibiti kambi ya kijeshi

Kwa mujibu wa maafisa wa uwanja wa ndege, ili kuhakisha kwamba vikosi vya Umoja wa Mataifa vinaondoka jeshi la Mali limetuma ndege mbili katika kambi ya Tessalit, zikiwa zimewabeba wanajeshi wa kundi la mamluki la Wagner kutoka Urusi.

Kambi ya Tessalit iko karibu na uwanja wa ndege na ilikuwa na wanajeshi wengi kutoka Chad chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa.

Kupitia mitandao ya kijamii jeshi la Mali limeandika ujumbe likiserma kwamba  ndege moja ilishambuliwa lakini ilifanikiwa kutua na kuondoka bila ya matatizo yoyote baada ya adui kudhibitiwa na jeshi la wanaanga.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walitaja shambulizi hilo lililotokea wakati wa asubuhi kama ishara ya  "kuzorota kwa kasi kwa hali ya usalama wa maisha ya mamia ya askari wa kulinda amani."

Mamlaka ya jeshi la Mali

Wanajeshi wa kikosi cha walinda amani nchini MaliPicha: Leon Neal/Getty Images

Jeshi la Mali, ambalo lilichukua mamlaka mnamo 2020, mnamo Juni lilitaka ujumbe huo wa walinda Amani wa Umoja Mataifa uliotumwa tangu 2013 kuondoka nchini humo licha ya kukabiliwa na wanamgambo wa itikadi kali na mzozo mkubwa wa pande nyingi.

Lakini uhamishaji wa kambi katika eneo la Kidal ambao ni ngome kuu ya wanaotaka kujitenga unatajwa kuwa katika kitisho kikubwa zaidi cha  kuongezeka kwa mgogoro.

Wanaotaka kujitenga hawataki MINUSMA irejeshe kambi hizo kwa jeshi la Mali kwa kuhofia kwamba ingekiuka usitishaji mapigano na makubaliano ya amani yaliyofikiwa na Bamako mwaka 2014 na 2015.

Mnamo Oktoba 2 jeshi la Mali lilituma msafara wa makumi ya magari, mengine yakiwa na silaha, kuelekea Kidal. Ukizingatia kwamba Kidal bado unadhibitiwa na waasi na eneo hilo linasalia kuwa changamoto kubwa kwa jeshi la Mali.

Majenerali wa jeshi wamerejesha mamlaka ya kitaifa na maeneo yote kuwa sehemu kubwa ya msukumo wake wa kutawala na kusisitiza kuchukua udhibiti wa kambi za Umoja wa Mataifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Mali Abdoulaye Diop mwishoni mwa juma alisema kwamba kujiondoa kwa Umoja wa Mataifa kutoka kaskazini mwa Mali kutafanyika kwa wakati na kutakamilika kufikia Desemba 31.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW